![]() |
| Advera Bulimba -SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi. |
Katika siku za hivi karibuni
kumeibuka tabia ya baadhi ya watu wachache wasiofahamika kutunga na
kusambaza ujumbe kupitia simu za mikononi na mitandao mbalimbali ya
kijamii wenye lengo la kuwatia hofu wananchi, jambo ambalo ni kinyume
cha sheria. Aidha, watu hao wanaosambaza taarifa hizo wanajifanya kwamba
taarifa hizo zimetoka kwenye taasisi za kimataifa na taasisi zingine
zinazoaminika jambo ambalo siyo kweli.
Jeshi la Polisi nchini linawataka
wote wenye tabia hiyo kuacha mara moja na badala yake, endapo mtu yeyote
anayo taarifa ya uhalifu wa aina yoyote ama kikundi chochote cha
uhalifu atoe taarifa hiyo katika kituo chochote cha Polisi au kupitia
simu za makamanda wa polisi wa mikoa ama vyombo vingine vya ulinzi na
usalama ili taarifa hizo ziweze kufanyiwa kazi haraka.
Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea
na uchunguzi wa taarifa zote zinazopokelewa ili kuhakikisha kwamba
usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.
Hata hivyo, Jeshi la
Polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kusambaza
ujumbe wenye mlengo wa upotoshaji, uchochezi ama kuwatia hofu wananchi.

No comments:
Post a Comment