SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limetangaza kuwa hakutakuwa na mgawo wa umeme katika maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Tanesco,
Felchesmi Mramba, alisema matengenezo yanayoendelea ya kusafisha visima vya
gesi asilia Songosongo hayataleta madhara yoyote wala kuwepo kwa mgawo wa
umeme.
Alisema
ni muhimu wananchi kufahamu kuwa matengenezo hayo yameshaanza na hakuna
usumbufu uliojitokeza wa kukatika kwa umeme.
“Naomba
wananchi mjue kuwa hatujatangaza mgawo wa umeme, bali kuna matengenezo ambayo
yanaendelea hivi sasa ya kusafisha visima vya gesi, hivyo ni kitu cha kawaida
wakati matengenezo yakiendelea kutokea matatizo madogo madogo yasiyoweza
kusababisha mgawo wa umeme,” alisema.
Mramba
alisema hali ya mitambo na miundombinu ya usambazaji wa umeme jijini imechakaa
hivyo kwa sasa wanajenga mipya yenye uwezo mkubwa zaidi wa kuhifadhi umeme.
Akivitaja
baadhi ya vituo vilivyokamilika kuwa ni Kipawa, Gongo la mboto, Mbagala na
Kurasini, ambavyo vimeshaanza kutoa huduma.
Akizungumzia
mvua zilizonyesha hivi karibuni, Mramba alisema zilisababisha baadhi ya nguzo
za umeme kuanguka na nyaya kukatika.
“Tulipata
matatizo mengi kipindi kile cha mvua, hivyo tumejitahidi kuzirekebisha nguzo zote,
ili wananchi wapate huduma kama kawaida,” alisema.
No comments:
Post a Comment