KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday, 19 April 2015

KINANA ASHIRIKI BONANZA

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akianza mazoezi wakati akishiriki  katika bonanza la Jogging lililoandaliwa na Kundi la Kaza Moyo Jogging Club la Ukonga Sitakishari ili kuhamasishwa vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura . 
 Mazoezi hayo yameanzia katika viwanja vya Gonga Gongo la Mboto kupitia Kipawa  na kuishia kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga ujumbe mkuu wa Bonanza hilo ulikuwa ni kuwataka vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata haki ya kupiga kura kuliko kuwa mashabiki tu.
Bonanza hilo la mazoezi limeshirikisha vilabu mbalimbali vya Joging kutoka mkoa wa Dar es salaam, Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mogo George Shinga Mtambalike, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida na kulia ni Bona Kaluwa Diwani wa Kata ya Kipawa.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)

No comments:

Post a Comment