KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday, 5 April 2015

LOWASSA: TUILINDE AMANI


Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Lowassa akiwa na waumini wengine katika Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Azania Front jijini Dar es Salaam juzi.
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewataka Watanzania kuilinda amani kwani ndio inawafanya wawe kitu kimoja

Lowassa, alitoa kauli hiyo, wakati wa Siku ya Ibada ya Ijumaa Kuu, iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Usharika wa Azania Front, jijini Dar es Salaam juzi.

Alisema ni jambo la kumshukuru mungu kwamba nchi kuwa inasherehekea siku hiyo ya Ijumaa Kuu ikiwa na amani na utulivu.

Lowassa, alisema kutokana na mazingira hayo, Watanzania wanapaswa kuienzi amani iliyoasisiwa na waasisi,  kwani bila ya amani wasingeweza kusherehekea siku hiyo wakiwa pamoja. 


No comments:

Post a Comment