![]() |
| Waziri Mkuu wa zamani, Sumaye |
WAZIRI Mkuu wa zamani Fredrick Sumaye amewataka Watanzania
kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi ili kuepuka mashambulizi ya kigaidi kama
yale yanayotokea Kenya.
Siku nne zilizopita nchini Kenya kumetokea mashambulizi ya
kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa, yaliyofanywa na Kikundi cha Al Shabab,
ambayo hadi sasa yanasadikiwa kuwa yameua zaidi ya watu 147.
Sumaye, alitoa kauli hiyo wakati wa ibada ya ibada ya Siku
ya Ijumaa Kuu, iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Azania Front,
jijini Dar es Salaam juzi.
Alisema hivyo kwa vile wapo baadhi ya Watanzania wanaodhani
kuwa mashambulizi kama yale hayawezi kutokea nchini wakiamini Tanzania ni nchi
ya amani.
Sumaye, alisema ili nchi iweze kuwepukana na mashambulizi
kama yale ni lazima kila mmoja kuwa
makini na watu wanaowatilia mashaka na kuacha dhana kwamba suala la ulinzi ni
la polisi au majeshi pekee.
“Tumeona hivi karibuni kuna kikundi cha watu kilijificha
kwenye mapango ya amboni na kuaanza kutishia amani ya nchi yetu, sasa ni lazima
watanzania tujenge umoja wa na tuwafichuwe watu hao wenye nia mbaya ya kuvuruga
amani yetu,”alisema Sumaye.
Licha ya mashambulizi nchini Kenya bado hapa nchini kuna
matatizo ya baadhi ya vituo vya polisi kuvamiwa na baadhi ya polisi kuuawa na
kuporwa silaha jambo ambalo linapaswa kuchukuliwa hatua za haraka ili kulikomesha.
Akizungumzia Ujumbe wa siku hiyo, Sumaye, alisema watanzania
wanapaswa kuonyesha upendo kwa baadhi ya watu wanaokabiliwa na matatizo.
Alisema hata Yesu aliteswa msalabani kwa ajili ya upendo wa
kuwasaidia wanadamu hivyo ni vema kwa kila mmoja kuepuka kuanzisha misuguano
kama vile mivutano ya wafugaji na wakulima.

No comments:
Post a Comment