Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa
Chama cha Mpira wa Miguu cha Afrika Kusini (SAFA) Dr.Danny Jordan
kufuatia kifo cha nguli aliyewahi kuichezea timu ya Taifa ya nchi hiyo
(BafanaBafana) John Lesiba “Shoe” Mashoeu kilichotokea jana Aprili 21.
Katika salamau zake kwa Dr.
Jordan, Malinzi amesema nchi ya Afrika Kusini imepatwa na pigo kubwa
katika tasnia ya mpira wa miguu, kufuatia kifo cha Mashoeu aliyefariki
dunia kwa ugonjwa wa Kansa ya Utumbo, na kusema watanzania wako nao
pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo.
John Lesiba “Shoe” Mashoeu
aliyezaliwa Disemba 18, 1965 nchini Afrika Kusini, alikuwa ni miongoni
wa wachezaji wa nchi hiyo waliotwaa Ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika
(AFCON) mwaka 1996 nchini Afrika Kusini na baadae kushiriki fainali za
Kombe la Dunia nchini Ufaransa mwaka 1998.
Wakati wa uhai wake Mashoe alipata
kuvichezea vilabu vya Giant Blackpool, Kaizer Chiefs, Amazulu na
Alexandria United vya Afrika Kusini, na timu Gencleribirligi,
Kocaeilispor, Fenerbahce na Busrsapor za Uturuki.
MASHINDANO YA COSAFA
Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi
za Kusini mwa Afrika (COSAFA) limepanga kuyaandaa na kuyatangaza
mashidano hayo yatakayofanyika mwezi Mei mwaka huu nchini Afrika Kusini
kwa mafanikio makubwa.
TFF inawaomba waandishi wa habari
wanaotaka kupata habari kuhusu mashindano hayo, watume mawasiliano yao
kwa Afisa Habari wa TFF.
Mawasiliano hayo ni: Jina Kamili, namba ya simu, barua pepe na kituo unachofanyia kazi
Taarifa hizo zitumwe kwa njia ya
barua pepe kabla ya siku ya ijumaa kumalizika, ili ziweze kutumwa kwenye
kitengo cha habari cha COSAFA.
NB: Kesho Alhamis saa 5 kamili
asubuhi kutakua na mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa
mikutano wa TFF- Karume, waandishi wa habari mnaombwa kuhudhuria.

No comments:
Post a Comment