Kamati za Kudumu za Bunge zitaanza
kukutana tarehe 27 Aprili hadi tarehe 4 Mei 2015 Jijini Dar es Salaam,
kutekeleza Majukumu yake, kabla ya Mkutano wa Bunge wa Bajeti uliopangwa
kuanza mjini Dodoma tarehe 12 Mei na kudumu hadi tarehe 25 Juni, 2015.
Kwa kawaida, Kamati za Kudumu za Bunge hupaswa hukutana wiki mbili kabla
ya Mkutano wa Bunge, ama Dar es Salaam, Dodoma au Zanzibar kuendana na
matakwa ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili 2013.
Hivyo, Wabunge wote wanapaswa kuwa wamewasili jijini Dar es
Salaam ifikapo Jumapili tarehe 26 Aprili 2015 tayari kwa kuanza vikao
siku ya Jumatatu tarehe 27 Aprili, 2015.
2.0 SHUGHULI ZITAKAZOTEKELEZWA
katika vikao hivyo Kamati 13 za Bunge zitajadili utekelezaji wa
Bajeti ya Serikali katika ngazi ya Wizara, Idara na Taasisi kwa mwaka
2014/2015 na mapendekezo ya mapato na matumizi kwa mwaka 2015/2016.
Siku ya Jumatano tarehe 28 Aprili,
2015 Wabunge wote kwa ujumla wao watakutana katika Ukumbi wa Julius
Kambarage Nyerere kupokea Mapendekezo ya Mpango, Kiwango na Ukomo wa
Bajeti ya Serikali ya 2015/2016 kwa mujibu ya matakwa ya Kanuni ya 97 ya
kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2013. Baada ya shughuli hiyo, Kamati
zote za Kisekta zitaendelea na uchambuzi wa Bajeti kuanzia tarehe 29
Aprili hadi 8 Mei, 2015
Pamoja na hayo, Kamati ya Bunge ya
Hesabu za Serikali itatumia muda huo kujadili Hesabu za Mikoa
zilizokaguliwa zinazoishia tarehe 30 Juni, 2013 na Kamati ya Bunge ya
Hesabu za Serikali za Mitaa itafanya ziara za ukaguzi wa thamani kwa
miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe
30 Juni, 2013 katika mikoa ya Dodoma na Singida.
Tofauti na kamati nyingine, Kamati ya Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa imeanza kazi zake mapema tarehe 20 Aprili, 2015 ambapo
inajadili Bajeti za Mikoa ya Tanzania Bara na Bajeti ya Wizara ya
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka 2015/2016.
3.0 SHUGHULI NYINGINE
Shughuli za Kamati zitamalizika tarehe 8 Mei, 2015 Jijini Dar es
Salaam ambapo Mkutano wa Bunge wa Bajeti utaanza tarehe 12 Mei, 2015
Mjini Dodoma na unategemewa kumalizika tarehe 25Juni, 2015. Ratiba za
shughuli za Kamati zote zitapatikana kwenye tovuti ya Bunge ambayo ni
www.parliament.go.tz
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
22 Aprili 2015

No comments:
Post a Comment