KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Friday, 24 April 2015

MPASUKO WAJITOKEZA NDANI YA TLP


Mwenyekiti wa TLP, Mrema

 MPASUKO ndani ya Chama cha TLP umejitokeza baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Agaustino Mrema kuwalazimisha Wajumbe wa Mkutano Mkuu waliokuwa wakipinga uteuzi wa  Katibu Mkuu wa Chama, Nancy Mlikaria, wa mkubali.
 Mpasuko huo umekuja baada ya wajumbe hao kupinga kitendo cha katibu mkuu wa anayemaliza muda wake kuteuliwa tena na mwenyekiti wa chama hicho huku akiwa mgombea pekee.
 Jana alfajiri katika Ukumbi wa Crystal Palace, Sinza jijini Dar es Salaam, wandishi wa habari ilishuhudia wajumbe hao wakimpinga mwenyekiti wao waziwazi kutokana na uwamuzi wake wa kibabe wakuwataka wajumbe lazima wamkubali katibu huyo.
 Mmoja wa wajumbe hao ambaye alianza kuzunguza bila ya kutaja jina, kutoka kanda ya Ziwa alisema katibu huyo hafai kwa vile hawezi kwenda sambamba na kasi ya ushindani wa vyama vingi.
 Alisema, kuwa katibu huyo wanampinga kutokana na tabia zake za kutokuwa na ushirikiano mzuri na wanachama walioko katika ofisi za chama huko mikoani.
 Mjumbe kutoka Mkoa wa Mara, alimuonya mwenyekiti kuwa kitendo chake cha kutaka arudishwe katika nafasi hiyo, atambuwe kuwa yatakapokuja kutokea yakutokea basi atambuwe kutakuja kuwajibika kutokana na natatizo ya katibu huyo.
 Mvutano huo wa kumkubali au kumtaa ulichukuwa zaidi ya saa 1 hadi pale Mwenyekiti wa chama, Mrema, alipowaomba wajumbe wa mkubali kwa kumpima kwa kipindi cha miezi sita.

Pamoja na ombi hilo la Mrema bado wajumbe hao waliendelea na msimamo wao wa kumkataa katibu huyo, hali iliyomfanya mwenyekiti huyo kutishia kuvunja mkutano huo.
 Kauli hiyo ilitafsiriwa wajumbe wenyeuzoefu na tabia za mwanyekiti huyo, kuwa kama kweli angevunja mkutano huo basi asinge wapa posho kitendo ambacho kingewaletea usumbufu wa kurudi makwao.
 Hata hivyo, kabla ya wajumbe hao kujibu, Mrema aliagiza kwa kusema wanaomkubali Nancy wanyooshe mkono juu, hali iliyo wafanya wengi kunyoosha, ikiashiria kuwa wamemkubali.
Baada ya kupitishwa kwa mbinde, Mrema alimuonya katibu huyo kuwa amesikia alivyolalamikiwa sasa ni wajibu wake wa kubadilika na kwamba hata kubali kuona anaiendesha ofisi ya chama anavyotaka.
 Nancy, alisema kuwa changamoto zote amezisikia akiahidi kuzifanyia kazi hususan kwa kushirikiana na wanachana wote.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ukweli na Maridhiano ya chama hicho, James Haule, alisema kilichofanyika ni kikao cha kupeana taarifa na si uchaguzi mkuu.
 Alisema kwa taratibu za uchaguzi ilitarajiwa kabla ya uchaguzi ilitakiwa achaguliwe mwenyekiti wa muda kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo.
Haule alisema baada hatua mbalimbali za uchaguzi kukamilika mwenyekiti huyo wa muda ndio angetangaza matokeo.
“Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa chama mwenyekiti wa uchaguzi ndio anatangaza matokeo hata kukiwa na mgombea mmoja hata kama amepigiwa kura ya hapana au ndio,”alisema Haule.
 Alisema, hayo yote hayakufanyika na kilichojitokeza ni Mrema, kusimamia shughuli zote za uchaguzi mwanzo hadi mwisho.
 Aidha, alisema kuna wananchama waliozuiliwa kugombea nafasi ya mwenykiti kwa kwa lengo la kumfanya Mrema amekosa mpinzani.
 Alisema mwanachama aliyezuiwa kwa madai kuwa amechelewa kurudisha fomu ni Mutamwega Mugaihwa, wakati sio kweli na cha kushangaza wapo waliokubaliwa kuchukua fomu hadi juzi asubuhi siku ya mkutano huo.
 Hata hivyo,  chama hicho kilikuwa hakijatangaza matokeo rasmi kutokana uchaguzi huo kumalizika jana alfajiri.

MWISHO




No comments:

Post a Comment