SERIKALI imesemasema kuwa imeridhishwa na maonyesho ya
madini ya vito yaliyoandaliwa na jumuia ya wafanyabiashara wa madini
nchini Tamida,kutokana na kuonyesha mafanikio makubwa yakiongozwa na
madini ya Tanzanite.
Waziri wa Nishati na
Madini,George Simba Chawene,ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua
maonyesho ya nne ya madini ya vito yanayoshirikisha wauzaji, wanunuzi
wakubwa wa madini hayo ulimwenguni .
Chawene,amesema kuwa hivi sasa
serikali ipo katika hatua za uimarishaji wa kiutengenezaji madini
ukataji wake na uchongaji hivyo kuyauza yakiwa yameongezewa thamani na
kutoa ajira nyingi tofauti na awali ambapo yalikuwa hayatoi ajira hizo
kutokana na kuuzwa yakiwa ghafi.
Amongeza kuwa serikali ipo
katika hatua za mwisho kutengeneza kituo kikubwa cha kuuzia madini
ambapo kutakuwepo na Hotel, maduka na ofisi za mamlaka ya mapato TRA, na
uwanja wa kutua Helkopta na hivyo kuondoa ulanguzi wa madinin na hivyo
kuongeza pato la taifa sanjari na kuondoa urasimu uliokuwepo wakati wa
mauzo ya madini.
Pia serikali itaweka vituo
maalumu vya ukaguzi kwenye machimbo ya Tanzanite,ili kudhibiti wizi
sanjari na kurejesha utaratibu wa kujenga ukuta uliokuwepo kwenye
machimbo hayo ambao ulibomolewa na baadhi ya watu wenye nia mbaya ili
waweze kutorosha madini hayo kwa urahisi ,pia kuimarisha ,utolewaji wa
vitambulisho .
Ameongeza kuwa utoroshaji wa
madini unaofanywa na watanzania ambao wamepewa leseni za kuuza na
kununua madini umepungua kutokana na udhibiti kuimarishwa.
Amesem,a miaka miwili iliyopita
Tanzania ilipata dola milioni 38 za kimarekani kutokana na mauzo ya
Tanzanite, huku Kenya ikipata dola milioni 100 kutokana na mauzo ya
Tanzanite, na India ilipata dola milioni 300.

No comments:
Post a Comment