WAZIRI wa Nishati na Madini, George Simbachawene, amevunja mkataba wa uwakala wa Kampuni ya
Selcom kutokana na mitambo yake ya kuuza Luku kuwa na matatizo ikiwemo matatizo
ya kisheria katika kulipa kodi.
Simbachawene alitoa kauli hiyo baada ya kulizwa swali na
wandishi wa habari kuhusu usumbufu wanaoupata wateja kila inapofika mwishoni mwa mwezi wanapotaka kununua huduma hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutembelea miradi
ya ujenzi ya vituo vya kutoa huduma ya nishati hiyo, Waziri huyo alisema kuna
kampuni mbili zilishinda zabuni ya kufanya kazi hiyo ya kuuza umeme kupitia
mashine za Luku ambazo ni Selcom na Max com.
“Nakuagiza mkurugenzi, kuiondoa kampuni hiyo na atafutwe mtu mbadala
ambaeye ataweza kufanya kazi hiyo na sio lazima afanye yeye amabaye ameshindwa
kutoa huduma kwa wananchi.
Simbachawene alisema anamtaka mkurugenzi huyo wa Tanesco
akamilishe mchakato huo haraka kwani tangu aingie katika wizara hiyo ni mara ya
tatu kusikia malalamiko hayo ambayo yanasabishwa na kampuni hiyo, jambo
linalowafanya wananchi washindwe kununua umeme na mwisho inayolaumiwa ni
Tanesco na Serikali.
“Hali hiyo inatokana na yule anayesimamia mauzo na kuuza umeme
mitambo yake ina matatizo lakini zaidi kuna masuala ya kiufundi pia kuna matakwa
ya kisheria kwamba lazina alipe kodi lakini kwa sasa wananchi waende kwa wakala
wa Max com amabaye mitambo yake haina matatizo,”alisema Simbachawene.
Simbachawene alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco kulishughulikia
suala hilo
baadala ya kumuacha aendelee kuchezea huduma hiyo muhimu kwa uchumi wa nchi.
Akizungumzia Miradi hiyo, Waziri, alisema baadhi ya miradi inayo
endelea kutekelezwa ni pamoja mradi wa Mbagala Megawati 100, Kurasani megawati
50, Gongolamboto Megawati 50, Kipawa Megawati 180 na Transmission line ya
kuunganisha vituo hivyo.
Simbachawene, alisema kazi zote hizo zinaendelea, baadhi
zimekamilika na nyingine zitakamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Aliongeza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutalifanya jiji la Dar es Salaam kuwa
miongoni mwa majiji yenye mfumo imara wa umeme katika Bara la Afrika.
Simbachawene, alisema kukamilika huko kutawahakikishia umeme wa
uhakika na kuondoa tatizo la kukakatika mara kwa mara kwa umeme katika jiji hilo.
Mkukurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba, alisema
licha ya matatizo hayo pia wamepokea maelekezo kutoka Malaka ya Mapatao
Tanzania (TRA), ya kuitaka Tanesco kufuta mkataba kati yake na Selcom, jambo
ambalo wameanza kulifanyia kazi tangu juzi.
“Tatizo la kukosekana
umeme halitokani na Tanesco bali linatokana Selcom hivyo tayari tumekwisha
mkatia huduma hiyo kutokana kwa hiyo hatunaye kwa maana hiyo serikali imevunja
mkata na serikali kutokana na kukwepa kulipa kodi,”alisema Mramba.

No comments:
Post a Comment