KATIBU
Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu, Mary Assay, amezitaka Wizara zote
kuufanyia kazi Mpango Kazi wa kitaifa wa
miaka mitano unaoanzia mwaka 2013 hadi
2017 kwa ajili ya uimarishaji haki za binadamu nchini kupitia malengo yake.
Assay,
alitoa kauli hiyo, wakati wa mafunzo ya siku moja ya kuwajenge uwezo waandishi wa
vyombombali vya hari jinsi ya kuripoti taarifa zinazo husu haki za binadamu,
yaliyofanyika jijini Dar es salaam leo.
“Unajua uelewa
wa masuala ya haki za binadamu nchini bado ni mdogo, haswa maeneo ya vijijini
ikiliganishwa na maeneo ya mijini,”alisema.
Assay, alisema
malengo hayo ni kuboresha hali sasa ya haki za binadamu kwa wananchi wote,
hususani masikini, wanyonge, jamii ya walio katika mazingira hatarishi na
waishio pembezoni mwa nchi.
Alisema
mpango huo utaongeza ufikikaji, kuaminika, uwajibikaji wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora na taasisi nyingine za kitaifa za haki za binadamu kwa
kuziimarisha na kuzipanua kiuwezo.
Aidha,
mpango huo umebainisha haki 23 zilizoko katika makundi manne ya ki-mada kama maeneo ya kipaumbele katika kuimarisha ukuzaji na
ulinzi wa haki za binadamu nchini.
Assay,
aliyataja makundi hayo kuwani Haki za kiraia na kisiasa, Kiuchumi, kijamii na
kiutamaduni, Makundi yenye mahitaji maalumu na kuimarisha taasisi na masuala
yaliyopo.
Aliongeza
kwa kusema kuwa tume hiyo ya haki za binadamu na utawala bora kwa kushirikiana
na Wizara ya Katiba na Sheria na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali
itafuatilia kwa karibu utekelezaji wa Mpango huo.
Awali akizungumzia
mafunzo hayo, Mratibu wa Mpango huo, Laurent Burito, alisema tume imeamua
kuwapatia mafunzo wandishi wa habari kwa vile anaamni watakapo uelewa vizuri itakuwa
rahisi kwao kufikisha ujumbe uliyo sahihi kwa wananchi.
Serikali
ya Tanzania
iliamua kuanzisha mchakato huo kwa mujibu wa mapendekezo ya Azimio la Viena la
mwaka 1993 na Programu yake ya utekelezaji katika kila serikali duniani.
No comments:
Post a Comment