KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday, 9 April 2015

WAPIGADEBE KITUO CHA MBEZI WAPIGA MADEREVA NA ABIRIA

Waziri wa Ujenzi, Dk. Maguful
VITENDO vya madereva na abiria kupigwa, kuporwa, kutolewa lugha za matusi na wapiga debe katika kituo cha mabasi Mbezi vimekuwa jambo la kawaida.
Kituo hicho kinasimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), wakati Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli alipokizindua alipga marufuku kuonekana wapiga debe, wauza magazeti na bodaboda ndani ya kituo hicho.
Hata hivyo agizo hilo, la Waziri Dk. Magufuli, limepuuzwa na wapiga debe hao, ambao wamekigeuza kuwa mali yao kwa kukiendesha wanavyotaka huku mamlaka ambazo zingeweza kuwadhibiti zikifumbia macho vitendo hivyo vya kihuni.
Wakati Dk. Magufuli akitoa agizo hilo, juzi usiku (saa 2:00), mwandishi ilishuhudia genge la wapiga debe wakilivamia gari la kifamilia T 445 CKM lililokwenda kituoni hapo kwa ajili ya kupokea ndugu zao waliokuwa wakitokea mikoani, wakidai wapewe sh 700 ambazo wameziita kwa ni za kitengo.
“Huu ni utaratibu wa kituo hiki kwa kila anayeingiza gari hapa lazima alipe unashangaa sh.700 mbona wapo wenzako wanalipa sh 500, 1000 na 200 sasa kwa vile ya kwako ni gari ndogo lazima uilipe hiyo tuliyokwambia,”alisikika mmoja wapigadebe hao.
Hata hivyo, mmiliki wa gari hilo ambaye jina lake halikupatikana alipinga kutoa fedha, hizo jambo lililowafanya wapigadebe hao waanze kuishambulia familia huku wengine wakijaribu kuwaibia lakini walishindwa.
Wapigadebe hao walitawanyika katika eneo hilo baada ya abiria waliokuwepo kituoni hapo kusanyika katika tukio hilo.
Mwandishi aliwashuhudia baadhi ya abiria wakiishauri familia hiyo kwenda kutoa taarifa polisi lakini ilikataa ikidai kuwa kila mmoja kati yenu ameona maonevu hayo, hivyo wanamuachia mungu ataamua.
Kati ya abiria aliyeshuhudia tukio hilo, alikuwa Khamis Jongo, ambaye alisema matukio ya kupigwa madereva na abiria katika kituo hicho yamekuwa yakijitokeza karibu kila siku lakini hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya wapigadebe hao ambao wengi ni watumiaji wa dawa za kulevya.
Alisema kuna kipindi walimpiga dereva ambaye hakuvumilia, alikwenda polisi ambapo ilijaribu kuwadhibiti kwa muda lakini hivi sasa wamerudi tena na kwamba wamekuwa wakifanya vitendo hivyo bila kificho jambo linalowashangaza madereva na abiria wanaotumia kituo hicho.
Hamisa Omari, alisema kuwa anawaomba polisi wa kituo cha Mbezi kuwaondoa kituoni hapo wapiga debe hao ambao wamekuwa kero katika kuwanyanyasa wanawake pindi wanapochagua gari la kupanda.

Alisema serikali inapaswa kuwa makini na wapigadebe kwani ni watu ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa kuliibia taifa kupitia fedha hizo wanazonyang’anya madereva kwani hazilipiwi kodi na kwamba wako katika kila kituo nchini.

No comments:

Post a Comment