Na MatukiodaimaBlog
WAKATI
watanzania wakijiandaa kushiriki kupiga kura yao juu ya katiba
inayopendekezwa wananchi wa kata ya Nsalala wilaya ya Mbeya
vijijini mkoani Mbeya wamedaia kuwa idadi ndogo ya nakala za katiba
zilizopelekwa katika kata hiyo wamekuwa wakilazimika kukusanyika
vikundi vya watu watano hadi kumi ili kusoma katiba hiyo ama
kuanzimana .
Wakizungumza na timu ya wanahabari wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP),
waliofika katika kata hiyo kufuatilia uelewa wa wananchi
juu ya katiba hiyo inayopendekezwa wakazi wa kata hiyo ya Nsalala walisema baadhi yao bado mzunguko wa kufikiwa na nakala
ya katiba chache zilizotolewa katika kata hiyo bado haujawafikia hivyo hawajasoma chochote.
Bw
Henson Mponi mkazi wa kijiji cha Nsalala kata ya Nsalala wilaya
ya Mbeya vijijini alisema kuwa ni vema serikali kuangalia
uwezekano wa kusambaza zaidi vijijini nakala za katiba hiyo
ili wananchi weweze kuzisoma na kuzielewa na kuwa haoni uharaka
wa kukimbiza zoezi hilo huku wananchi wakiwa gizani .
Alisema
kuwa bunge la katiba limemaliza kazi yake ya kuandaa katiba hiyo
hivyo ni zamu ya wananchi nao kupewa muda wa kuipitia na
kuielewa kabla ya kupita kura kwa jambo ambalo wao hawalitambui.
Kwani
alisema hadi sasa kijiji chake cha Nsalala chenye watu 701
nakala za katiba ambazo walitangaziwa kuwa zimefika ni 36 huku
kitongoji cha Nsalala chenye watu 150 wamepewa nakala 5 za
katiba hivyo shida ya kusoma inatokana na idadi ndogo ya nakala
za katiba hizo na kupelekea wananchi kuanzimana ama kusoma kwa
makundi makundi .
Alisema
kuwa wanachoshukuru ni kufikiwa mapema kwa katiba hizo ambazo toka
mwezi wa pili wananchi walipewa katiba hizo ila hadi sasa bado
mzunguko wa kufikiwa na nakala za katiba hizo ni mgumu zaidi.
"Tunaomba kuongezewa nakala zaidi za katiba kwani vinginevyo
shughuli za uzalishaji mali kwa wananchi wakulima hapa kijijini
zitayumba zaidi kutokana na kusubiri kukusanyika kusoma katiba
hiyo…ushauri wangu ni vema nakala za katiba zingeletwa kulingana
na idadi ya wananchi kama tupo 150 basi nakala 150 zingeletwa ili
kila mmoja aweze kuwa na nakala yake na kutenga muda wake wa
kuisoma kuliko kusubiri kupokezana ama kukusanyika makundi"
Hata
hivyo alishauri kama inawezekana serikali kuzileta katiba nyingi
zaidi na kuziuza kati ya Tsh 10,000 ama 20,000 ili wananchi waweze
kununua wenyewe na kujisomea kuliko hizo za bure ambazo hazitoshi
kulingana na idadi ya watu katika kata na vijiji vya kata hiyo.
Bw
Aron Zambi ni mjumbe wa serikali ya kijiji cha Nsalala alisema
kuwa hajafahamu kuwa serikali imegawa nakala hizo za katiba
kwa kuanglia uwiano gani kutokana na kusambaza idadi ndogo zaidi
za nakala za katiba hiyo .
Zambi
alisema kuwa ni vema wananchi wakasoma katiba hiyo badala ya
kutegemea wana siasa wawahamasishe kuipigia kura ama kutoipigia
kura kwani alisema anachokiona yeye ni mwisho wa siku katiba
hiyo kupigiwa kura ama kutopigiwa kura ya ndio kutokana na wengi
wao kutoisoma.
Kwani
anasema hata hatua ya tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kusogeza
mbele zoezi la kura za maoni bado halitasaidia kwani kama nakala
za katiba zaidi hazitasogezwa kwa wananchi hata kama zoezi hilo
litasogezwa hadi mwakani kama wananchi hawana nakala za katiba
mkononi uwezekano wa kuzitafuta wenyewe hautakuwepo hivyo ni sawa
na bure.
Afisa
tendaji wa kijiji cha Nsalala Bw Lwitiko Mwaidindi alisema
kuwa alipokea nakala 36 pekee za katiba wakati kijiji hicho
kinajumla ya wananchi wenye umri wa kupiga kura 701 .
Afisa
mtendaji kata ya Nsalala Bw Joseph Stima alisema kuwa kata
yake inajumla ya wapiga kura 19,346 wakiwemo wanaume ni 9143 na
wanawake ni 10203 ila idadi ya nakala za katiba inayopendekezwa
waliyoipata ni 261 pekee na kuwa nakala hizo zimesambazwa katika
vijiji vyote pamoja na makundi maalumu kama wanawake ,walemavu,
taasisi mbali mbali na maeneo mengine yenye mikusanyiko mbali
mbali pamoja na viongozi wa vitongoji vyote 6 vya kata hiyo
ambavyo ni Tunduma Road , Mshikamano,Mapinduzi , Ndola na Nsalala
kulingana na idadi ya watu katika vitongoji hivyo..
No comments:
Post a Comment