KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday, 2 April 2015

ZAIDI YA WATU 15 WAUAWA KATIKA CHUO KIKUU GARISSA

 Serikali ya Kenya kupitia waziri wa mambo ya ndani, Joseph Nkaiserry, amesema kuwa watu 15 wameuawa na wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa katika shambulio lililoendeshwa na watu wenye silaha katika Chuo kuu cha Garissa, Mashariki mwa Kenya. kilomita 150 na mpaka wa Somalia.

Mpaka sasa bado kuna watu ambao wameendelea kushikiliwa mateka katika hicho.

Serikali ya Kenya imemtaja Mohammed Kuno ambaye anajulikana kwa jina la Gama Adhere kama mshukiwa aliyepanga shambulio hilo, ambalo limegharimu mpaka sasa maisha ya watu 15.
Serikali ya Kenya imetoa zawadi nnono ya dola 53,000 kwa atakayemkamata Mohammed Kuno au atakayetoa taarifa kuhusu mshukiwa huyo.

Wakati huohuo Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ametuma risala za rambi rambi kwa familia za watu waliouawa katika shambulio lililotokea katika chuo kikuu cha Garissa mashariki mwa Kenya.Rais Uhuru Kenyatta pia amewahakikishia raia wa Kenya kuwa serikali yake imechukua hatua ya kuongeza vikosi vya usalama katika eneo hilo.

Rais Kenyatta amewatolea wito raia wa Kenya kuwa watulivu, wakati vikosi vya usalama vikiendelea na operesheni ya kuwaska washambuliaji.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya, shambulio hilo lilianza saa za swala mapema asubuhi, kwenye majira ya saa kumi na moja na nusu leo Alhamisi. Idadi ya watu walioendesha shambulio hilo haijajulikana

Kwa mujibu wa gazeti la Kenya la The Standard, wanafunzi waliofaulu kuondoka chuoni hapo, wamesema waliwaona watu watano wenye silaha.

Kwa mujibu wa polisi ya Kenya, watu hao wenye silaha, walianza kufyatua risase walipoingia chuoni hapo.

No comments:

Post a Comment