KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Friday, 22 May 2015

HATIMAYE AMI YAKABIDHIWA KWA MMILIKI

Meneja Biashara wa Kampuni ya Udalali ya Mem, Elieza Mbwambo (kulia), akimkabidhi funguo Meneja wa Kampuni ya Navtej Bains, Zulfiqar Hassanali, baada ya kampuni hiyo kuwaondoa wapangaji Hospitali ya Ami waliokuwa na deni la sh. bilioni 3. Makabidhiano hayo yalifanyika nje ya jengo hilo Oysterbay jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Francis Dande).    
HOSPITALI maarufu kwa kutibu vigogo wa serikali, African Medical Investment (AMI), hatimaye imefutwa rasmi baada ya jengo la hospitali hiyo kukabidhiwa kwa mmiliki wa jengo hilo kwa nguvu ya mahakama.
Nao wafanyakazi wa hospitali hiyo wamesema hawajui hatima yao, baada viongozi wao kuzima simu zao.
Hali hiyo ilitokana na mri ya Mahakama Kuu kuagiza mali za hospitali hiyo zikamatwe na jengo la hospitali hilo lirejeshwe kwa mmiliki wake kutokana na kushindwa kulipa kodi ya pango sh. bilioni 3.2 kwa zaidi ya miezi 26.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam le, Meneja Masoko wa Kampuni ya Madalali (MEM), Elieza Mbwambo, alisema kazi yao ilikuwa ni kukamatama mali na kukabidhi jengo, masuala ya kudai fedha ni jukumu la mmiliki.
Alisema kuwa walifikia hatua hiyo baada ya uongozi wa hspitali hiyo kutii amri ya mahakama ya kuwaondoa wagonjwa wote na kwamba mali walizokamata wataziuza.
“Wiki mbili zilizopita tulikuwa hapa kukamata mali na tuliwapa taarifa wagonjwa wote waliokuwa hapa waondoke na leo tunashukuru wagonjwa wote wameondoka na leo tunamkabidhi jengo mwenye mali,”alisema Mbwambo.
Mbwambo, alisema vifaa vyote vilivyokamatwa vitaviuzwa, hata hivyo, fursa itatolewa kwanza kwa mmiliki wa jengo hilo.
Akizungumza kwa niaba ya Kampuni ya Navtej Singh ambao ndiyo wa jengo hilo, Zulfiqar Hassanali, alisema baada ya kukabidhiwa jengo lao, wanatarajia kufungua hospitali kama mwanzo kwa vile eneo hilo la Msasani halina huduma hiyo zaidi hapo.
“Bado hatujampata mtu kwa sababu baada ya kutokea tukio hili kuna watu wengi wamejitokeza kuomba jengo hili kwa kuendesha shughuli hizi,”alisema Hassanali.

Wafanyakazi

Msemaji wa Wafanyakazi, Roselin Sesoa, alisema walishangazwa na hatua hiyo kwa vile ongozi uliendesha mgogoro kwa usiri mkubwa ambao hawakuwa kuujua.
Alisema, kutokana na mazingira hayo, wanashindwa kujua hatma ya haki zao kwamba watazipata wapi kwani uongozi wa hospitali hiyo haupatikani na wala hawajui waliko kimbilia.
“Unajua tuko 100 ambao hatujui jinsi ya kupata haki zetu kwani tangu kutokea kwa tukio hili viongozi hawajulikani waliko tukiwapigia simu hazipokelewi na hawa ni wageni,”alisema Sesoa.
Sesoa, aliitaka serikali kuwa makini katika kutoa fursa za uwekezaji kwa wageni kwani kama hawa wangekuwa wenyeji naamini serikali ingeweza kuwafuatilia kirahisi katika kusaidia wapate haki zao.


No comments:

Post a Comment