![]() |
| Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philp Mangula |
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi (UVCCM), wilayani Rufiji, Pwani, Shaban Matebwe, amesema wako watu
wanaokichafua chama hicho kwa kushiriki waziwazi katika utoaji rushwa ili
wapate kuchaguliwa kwenye nafasi za uongozi.
Alisema hivyo kwa vile kuna watu wanaokwenda wilayani
hapo kuinadi rushwa waziwazi kwa ajili ya kutaka kuteuliwa na chama ili waje
wagombee nafasi ya ubunge na udiwani wakati wa Uchguzi Mkuu unaotarajiwa
kufanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es
Salam leo, Matebwe, alisema kuna ulazima wa watu hao wakatambua kuwa msingi wa
chama hicho ni kuwatetea wanyonge na masikini hivyo hakitakubali kutoa nafasi
kwa wala rushwa.
Alisema hivyo kwa kuwa sheria ya uchaguzi ya
mwaka 2010 inakataza wagombea wanafasi ya uongozi katika chama chochote kutoa
rushwa, kwa maana hiyo mgombeya yeyote atakaye bainika ametoa rushwa, anaweza
kukatiwa rufaa ya kutokuwa mgombea.
“Mgombea wa chama chochote akitoa rushwa ili
achaguliwe katika nafasi ya uongozi ikibainika kweli ametoa rushwa inawezekana
kabisa akatiwa rufaa ya kutokuwa mgombea,”alisema Matebwe.
Matebwe, alisema kutokana na sheria hiyo,
wanachama wa CCM wanapaswa kujihadhari na wagombea wa aina hiyo kwani wanaweza
kuja kukipotezea nafasi chama pindi watakapo katiwa rufaa na wapinzani.
Alisema ili kuepuka hayo yasije kukikumba chama,
ni vema uongozi wa juu ukatoa onyo ambalo litawafanya watu hao wasiendelee
kukichafua na kukidhalilisha chama hicho.
Aidha, alisema kama watu hao wataendelea
kukichafua chama kwa mtindo huo basi UVCCM wilayani Rufiji itawaweka hadharani
watu hao ambao wanalinyemele jimbo hilo.
Jimbo hilo
la Rufiji kwa sasa liko chini ya Seif Rashid ambaye ni Waziri wa Afya na Ustawi
wa Jamii.

No comments:
Post a Comment