![]() |
| Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi |
DIWANI
wa Kata ya Somangila Aisha Mpanjila, amemtahadhalisha Mwenyekiti wa Kijiji cha
Mbutu, Kigamboni wilayani Temeke jijini Dar
es Salaam, ahakikishe anaitafutia ufumbuzi migogoro ya
ardhi kwa kuzingatia sheria na haki.
Aisha,
aliitoa kauli hiyo jijini juzi, wakati wa mkutano wa hadhara ambao ulifanyika
viwanja vya kijiji hicho, ulitawaliwa na malalamiko yanayohusu migogoro ya
ardhi ya muda mrefu.
Alisema
hivyo, kwasbabu kama atashindwa kutatua
migogoro hiyo kwa kuzingatia sheria na haki basi atambue kuwa itamueka katika
mazingira magumu na itamshinda kitendo kitakachofanya wananchi washindwe kuwa
na imani naye.
Aisha,
alisema mfano wa migogoro hiyo ni ule wa shamba la Kijangwamiya, ambao bado
unaonekana kuwachanganya wanakijiji kwamba hadi sasa hawamjui mmiliki halali wa
shamba hilo.
“Ukiangalia
utaona kuwa suala la mgogoro wa shamba hilo la
kijiji cha Kijangwamiaya halijapatiwa ufumbuzi kutokana na wananchi kuuliza
maswali kuwa shamba hilo
ni lao au ni la nani,”alisema Aisha.
Alisema
kwa vile bado kuna maswali mengi kutoka kwa wananchi kuhusu shamba hilo basi ni vema
akaendelea kulishughulikia kisheria ili ukweli ujulikane kuwa ni nani mmiliki
halali.
Naye
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Jamal Mfaume, alisema wakati anaingia katika
uongozi wa kijiji hicho, alikabidhiwa nyaraka ambazo zinaonesha kuwa shamba hilo ni la kijiji hicho.
“Unajua
mimi nimeingia ni kakuta mikataba mbalimbali amabyo ilikuwa imeishaingiwa
kisheria na uongozi uliyopita hivyo unaweza kuona kinachoendelea hapa,”alisema
Mfaume.
Mafaume,
alisema wakati anaingia katika uongozi amekuta migogoro mingi ya ardhi ambayo
baadhi yake iko mahakamani hata hivyo, aliahidi kuwa ataishughulikia kwa
kuzingatia sheria na haki.
Aidha,
mkutano huo ulitawaliwa na itikadi za vyama jambo ambalio limfanya mmfanya
mmoja wa wanankijiji hicho, Yeiko Nyerere, kuwatahadharisha wenzake kuwa waache
kuchanganya masuala ya maendeleo na siasa.
Alisema
kama wanakiji hao wataendekeza mihemuko ya kitikadi ya vyama vyao basi
watambuwe kuwa maendeleo katika kijiji hicho yakuwa ndoto kwao.

No comments:
Post a Comment