![]() |
| Kushoto ni Mwakilishi wa Uzini Raza, akiwa na Ofisa wa Idara ya Habari Maelezo Tiganya, wakati alipozungumza na wandishi wa habari hawako pichani |
Tanzania hivi sasa iko katika harakati za Uchaguzi Mkuu ambao
unatarajiwakufanyika Oktoba mwaka huu.
Raza ambaye ni Mwakilishi
wa Uzini, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, wakati alipozungumza na
wandishi wa habari, kuhsu mustakakabali wa kupatikana Rais wa Jamhuri ya
Muungano kwa vile hilo ni suala nyeti katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi
mkuu.
“Suala hili lina unyeti wake
kwani linagusa hadi majeshi na mahakama amabao nao wanapaswa kujua sifa za rais
ajaye, hivyo haitakuwa busara kwa rais wa nchi apatikane kwa njia ya rushwa.
Alisema hivyo kwa vile kuna
baadhi ya wawagombea wanafasi hiyo, wakishirikiana na wafanyabiashara tayari
wanaendelea na mchezo huo mchafu wa kutoa rushwa waziwazi huku hata Kamati Kuu
ya Chama Ikishindwa kukemea vitendo hivyo vya hatari kwa nchi.
“Nazungumzia chama changu,
tumeingia kwenye uchaguzi mkuu, naamini bado tunakazi ya kutekeleza Ilani ya
chama cha mapinduzi hatujamaliza kazi, sasa kama
sisi viongozi tunaona mabilioni ya rushwa yakiingizwa dhahiri bila ya kukemewa
imenishtua,”alisema.
Raza, alisema kitendo cha
kupatikana rasi iliyetokana na misingi ya rushwa, itafika wakati rais huyo
atashindwa kuwa na maamuzi ya kuongoza nchi na baadala yake atakuwa akitekeleza
matakwa ya magenge ya watoa rushwa.
“Tunapompata rais ambaye
amechaguliwa kwa misingi ya rushwa Watanzania wajue kuwa atakuwa akielezwa na
waliomuingiza madarakani kwamba mchague huyu au yele ashike wizara fulani kwa
ajili ya maslahi yao,
lakini pia chama changu lazima kijue kuwa kuna Ukawa na CUF ambao nao wanataka
kuingia madarakani,”alisema Raza.
Akizungumzia Suala Akaunti ya
Tegeta Escrow, Raza, alisema kuwa Wazanzibar wanamtaka Waziri wa Fedha, atoe
tamko atalifidiaje pengo Zanzibar
kukosa misaada kutokuna naTanzania kuwekewa vikwazao na wahisani kutokana na
kashfa ya Akaunt ya Tegeta Escrown.
Alisema, hivyo kwa vile
kashfa hiyo haiwahusu Wazanzibari, kwani
halikuwa suala la muungano bali lilikuwa la Bara.
Hata hivyo, Raza, alisema bado
viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibarr, wanatakiwa kuacha woga na baadala
yake wajenge hoja kwa kuwaambia wahisani kuwa suala hilo haliwahusu Wazanzibari.
“Mwaka 1995 Zanzibar,
iliwekewa vikwazo na huku bara ikidai kuwa iliambiwa na wahisani isiwape
misaada, lakini kwa hili la Escro, viongozi wa Zanzibar walitakiwa kujenga hoja kwamba
haliwahusu, angalia pale hakukua hata na Mzanzibari aliyehusika katika kashfa
ya Tegeta Escro,”alisema Raza.
Raza, alisisitiza kuwa hata
wakati wa EPA wazanzibari hawakuhusika lakini waliingizwa akibainisha kuwa hayo
yote yanatokea kutokana na woga wa viongozi wa Serikali ya Zanzibar.
Aidha, Raza amesistiza kuwa
alifuatilia suala hilo la vikwazo ili
ikiwezekana Zanzibar
iweze kuondolewa vikwazo hivyo ambavyo anaamini haviihusu Zanzibara.

No comments:
Post a Comment