CHAMA cha Wananchi (CUF), Kata ya Kigogo wilayani Ilala Dar es Salaam leo kimepiga kura ya maoni kwa ajili ya kupata mgombea atakayeweza kupambanishwa na wagombea wengine wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Vyama vinavyo unda umoja huo ni
Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NLD na
NCCR-Mageuzi.
Akizungumza na wandishi wa
habari kuhusu mchakato huo, Katibu Kata wa CUF Kata ya Kigogo, Khalid Singano
ambaye pia ni mgombea wa chama hicho, alisema walichofanya ni hatua ya awali.
Alisema baada ya kura hiyo ya
ndani mshindi atashindanishwa na wagombea wengine kutoaka vyama vinavyounda
umoja huo kwa ajili ya kumpata mshindi wa jumla atakayepambana na yule Chama
Cha Mapinduzi (CCM).
“Vigezo vitakavyotumika kumpata
mshindi huyo wa jumla, itaangaliwa takwimu za vyama vyote zinazohusiana na
chaguzi mbalimbali zilizopita, kukubalika kwa chama na kukubalika kwa
mgombea,”alisema Singano.
Singano, aliwataja wagombea hao
kuwa ni Mwinyi Madenge, Baraka Nyakite,
Iddi Maza, Sellemani Sellemani pamoja na yeye mwenyewe (Singano).
Alisema upepo wa kura hizo za
ndani ulikuwa ukiangalia zaidi uwezo wa watendaji ambao wameweza kukisaidia
chama na kukifanya kipate mitaa mitatu katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka
jana.
“Sio dhambi mimi ni miongoni
mwa watendaji wa chama hiki tuliyoshiriki katika kukiimarisha katika kata hii
ya kigogo kwa hiyo uwezo wa kuongoza kata ni nao,”alisema.
Hadi gazeti hili linakwenda
mitamboni matokeo yalikuwa bado hayajatangazwa.
No comments:
Post a Comment