|
WAZIRI wa
Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu) Dk. Mary Nagu kuacha kufanya
kampeni mapema kabla ya chama hakijatoa tamko rasmi la kuwataka wanachama
wake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Dk. Nagu ambaye
ambaye pia ni Mbunge wa Hanang’ mkoani Manyara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),
alitoa juzi wakati alipozungumza na wandishi jijini Dar es Salaam juzi.
Alitoa
maelezo hayo kufuatia kutolewa kwa kauli ya kuwataka wakazi wa
Hanang, kumuunga mkono mwanasheria wa Kampuni ya FW Law Chambers Advocates
ya jijini Dar es Salaam, Duncan Mayomba kama
ataridhia ushauri wa Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye wa kugombea
Ubunge katika jimbo hilo.
Hivi
karibuni Sumaye katika mkutano wa hadhara uliofanyika Hanang’ aliwataka
vijana wasomi, akiwemo Mayomba, kujitokeza na kugombea Ubunge katika jimbo hilo.
Waziri
Dk. Nagu alisema ni mapema mno kufanya kampeni wakati huu, kwani
kufanya hivyo ni kukiuka maadili na taratibu zilizowekwa na Chama kwa
wanachama wake.
Taratibu
hizo kwa mujibu wa Dk. Nagu ni kutokushiriki katika kufanya
kitendo cha aina yoyote kile kitakachoashiria kufanya kampeni
mapema mpaka hapo Chama cha mapinduzi kitakapotangaza rasmi.
“Ninasikitishwa
sana na mambo yanayotokea Hanang’ nashindwa
kupata picha halisi kama ni kweli mtu
unayemheshimu kufanya vitendo vinavyofanywa na kiongozi wa
kitaifa kuendesha kampeni ya kuwashawishi wananchi kumchagua mtu
anayemtaka yeye kwa maslahi yake na wala siyo kwa maslahi ya watu wote”,
alisema Dk. Nagu.
Alisema kuwa
haogopi wala hatishwi na matendo yanayofanywa jimboni kwake, lakini kitu
kikubwa kinachomfanya kujiamini ni pamoja na kutembea kifua
mbele kwa wananchi wake kutokana na jinsi alivyotumia vizuri muda
wake mwingi jimboni humo katika kutekeleza kivitendo Ilani ya (CCM).
Aidha,
alisema kuwa kutokana na imani hiyo ndiyo iliyosababisha kuteuliwa kuwa
Mjumbe wa Halmashauli Kuu ya (CCM) MNEC.
Dk.
Nagu alisema kuwa wananchi wanahitaji maendeleo na siyo sifa ya mtu, eti
kwa sababu kijana au msomi. “Wananchi wanataka maji, shule bora,
miundombinu imara na huduma bora za kiafya kama hospitali na dawa ili
yawasaidie katika kuboresha maisha yao”,
aliongeza.
“Nimeweza
kujitahidi kadri ya uwezo wangu kutekeleza mambo yote muhimu yanayohitajika
kwa wananchi.
“Nimetumia
nafasi zangu serikalini kuwashawishi wawekezaji kuwekeza jimboni kwangu,
nimefanikisha kufanyika kwa miradi mikubwa ukiwemo ule wa kuwapatia
wakulima matrekta”.
Kiongozi
huyo wa serikali alisema kuwa ameweza kuanzisha vikundi vingi
vya akinamama vya Kuweka na Kukopa (VICOBA) pamoja na SACCOS,
kuanzisha vikundi vya vijana vya kilimo cha kisasa na kuwapatiwa matrekta
na pembejeo.
|
No comments:
Post a Comment