KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday, 7 May 2015

WASIRA: HAKUNA UHABA WA CHAKULA

WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, amesema hali ya chakula nchi ni yakuridhisha.
Wasira alitoa kauli hiyo, juzi wakati wa akipokea msaada wa tani 7,492.7 za mbolea ya urea wenye thamani y ash. bilioni 5.7 kutoka nchini Japan.
Alisema hivyo kwa vile hadi sasa nchini kuna zaidi ya tani 300,000 za chakula ambazo zinaweza kusaidia kuziba pengo katika maeneo mengine ambayo yanaweza kukumbwa na upungufu wa chakula.
“Unajua kuna kipindi kama hiki cha mwezi Mei inaweza ikatokea upungufu wa chakula, lakini kinakuwa kipindi kifupi kwani wakati huo wanajiandaa na msimu wa mavuno,”alisema Wasira.
Wasira, alisema hali ya chakula mashambani katika mikoa 16 hivi sasa ni nzuri, hivyo basi serikali inajiandaa wakati ukifika Julai mwaka huu itaanza kununua mazao hayo.

“Kupanda kwa bei ya chakula kunakuwa kwa muda mfupi hususan katika kipindi cha Mei, mara baada ya kuvuna Mwezi Julai hali hurejea katika hali ya kawaida,”alisema Wasira.
Akizungumzia msaada huo wa mbolea, Wasira alisema mbolea hiyo itasambazwa katika maeneo mbalimbali ya nchini kwa ajili ya kuimarisha hali ya uzalishaji wa chakula.
“Tumekuwa na ushirikiano na Japan katika miradi mbalimbali ya kilimo tangu mwaka 1978,”alisema Wasira.
Naye Balozi wa Japani nchini, Masaharu Yoshida, wakati akikabidhi msaada huo, alisema anatarajia kuwa msaada walioukabidhi, usiishie kusambazwa bali ulete matokeo chanya.

Alisema, msaada huo, utaongeza kasi ya uzalishaji wa chakula kitendo kitakachosaidia kupunguza umasikini na kufanya nchini iwe salama zaidi kichakula.

No comments:

Post a Comment