KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday, 10 May 2015

PAC YAUAGIZA MKOA WA MARA KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA YA MKUU WA WILAYA YA SERENGETI



KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeuagiza uongozi wa Mkoa wa Mara kuharakisha ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Serengeti ili kukomesha matumizi mabaya ya fedha za serikali kwa kumlipia kodi ya kuishi hotelini.
Mkuu huyo wa wilaya ameishi hotelini kwa zaidi ya miezi miwili tangu alipoteuliwa na kwamba hadi sasa ametumia zaidi ya sh. milioni 600.
Akizungumza juzi jijini wakati wa kujadili taarifa za mkoa huo wa Mara, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati, hiyo, Aden Rage, alisema kitendo cha kumuacha mkuu huyo wa wilaya kuendelea kuishi hotelini hakileti picha nzuri. 
Alisema kutokana na kamati hiyo kutoridhishwa na taarifa hiyo ambayo ilikuwa ikionesha kilichobaki katika ujenzi wa nyumba hiyo ni tenki la maji ni vema mkoa huo ukakamilisha kazi hiyo mara moja.
Rage, alisema kuwa kamati hiyo inauagiza ungozi wa mkoa huo kamilsha kazi hiyo na kufikisha nakala katika ofisi ya CAG, Ofisi ya Bunge na kamati yenyewe.
Kamati hiyo iliutaka uongozi wa Mkoa wa Mara kutumia utaratibu na sheria sahihi wa manunuzi ya serikali ili kuepusha wizi na ubabaishaji unaoweza kutokea.
Katika hatua nyingine Kamati hiyo haikuridhishwa na taarifa za utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2014/2015, kutokana na kuwa na mapungufu mengiAkizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge jijini Dar Salaam mara baada ya kumaliza vikao vya wiki mbili za kupitia taarifa hizo, Rage alisema kwamba katika kuzikagua hesabu za mikoa yote zilibainika kuwa na hati za mashaka.
“Mikoa yote ina hati za mashaka kwa sababu katika kukagua taarifa zao, mara utaona milioni kadhaa zimeliwa bila maelezo ama milioni kadhaa zimeingizwa katika matumizi yasiyokuwa yake au hakuna nyaraka za matumizi huiska” alisema Rage
Alitoa mfano wa mikoa miwili wa Mara na Tanga ambayo walikuwa wakiijadili kwa siku ya jana kama hitimishwa kwamba nayo imefanya vibaya katika taarifa yake .
Kauli ya wabunge wa kamati hiyo imetokana na manunuzi feki katika vitu mbalimbali yaliyofanywa katika Hospitali ya Mawezi ambapo fedha zaidi ya mil 20 za kununulia mashine ya kufulia  zimeliwa bila kufanyia kazi iliyopangwa pamoja na kununua dawa nje ya Bohari Kuu ya Dawa  (MSD).
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hery Ally Khamis alisema juzi kuwa licha ya kutakiwa kufuata utaratibu huo pia watekeleze maagizo waliyokwisha yatoa katika kipindi cha mwaka 2012 ikiwa ni pamoja na aliyetapeli fedha za kununulia mashine ya kufulia katika hospitali ya Mawenzi kuzirudisha.
Wakichangia hoja hiyo Mjumbe wa kamati hiyo Ismail Aden Rage alisema kuwa uongozi wa mkoa ulitaka hapo awali suala hilo lisikilizwe nje ya mahakama na kukubaliana kulipwa kwa fedha hizo lakini hadi leo kati ya mil 20 imelipwa mil 3 tu jambo ambalo ni ubabaishaji.
Naye Mjumbe Ally Kessy alisema aliyetakiwa kulipa mil 20 ilikuwa kwa miaka mingi iliyopita hivyo akashauri akianza kulipa aweke na riba.
Hata hivyo Mjumbe ambaye ni Mbunge wa Kibiti Abdul Malobwa alishangazwa na bajeti ya Mkoa wa Kilimanjaro kupatiwa fedha nyingi za bajeti hadi na ziada na kurudishwa hazina huku mikoa mingine ikiwa haina fedha za kutosha.
Katika hilo RAS hakuwa na majibu na kutakiwa atakaporudi tena kutoa majibu huku wabunge hao wakihoji kama kuna mtu hazina anawaunganishia na kupata kiasi hiko kikubwa cha fedha.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, (RAS) Severine Kahitwa alizungumzia utapeli wa mil 20 na kusema kuwa walipogundua kuwa ni tapeli waliamua kumpeleka mahakamani  na walipoona kuwa hawakufanya sahihi walishauriana nje ya mahakama na mtu huyo kuanza kulipa fedha hizo.
Hata hivyo alisema tayari wameanza kujirekebisha na kufuata utaratibu wa manunuzi kama serikali inavyoagiza sambamba na kumfuatilia aliyechukua mil 20 kurudisha kwa wakati.
wisho


No comments:

Post a Comment