KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 11 May 2015

FILIKUNJOMBE AKABIDHI MSAADA WA TSH MILIONI 40 KIJIJI CHA MAVANGA ASEMA CCM SI MBAYA WABAYA WATU

Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo  Filikunjombe akiwhutubia  wakazi  wa  kijiji  cha Mavanga  wilayani Ludewa  muda mfupi  baada ya  kukabidhi msaada wa  vitu mbali mbali  vya  ujenzi vyenye thamani ya Tsh milioni 40 katika  kijiji hicho


Na MatukiodaimaBlog

MBUNGE 
wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe amesema baadhi ya 
wabunge, mawaziri na watendaji wabovu serikalini wanakichafua chama cha 
mapinduzi ( CCM ).
 
Filikunjombe, alisema kuwa 
CCM ni chama makini na kinachopendwa ila shida ipo kwa baadhi ya 
watu waliopo ndani ya CCM na serikali ambayo ni bomu.
Mbunge 
huyo alitoa kauli hiyo leo  katika kijiji cha Mavanga wakati akijibu 
maswali ya wananchi na viongozi wa Vyama vinavyounda Katiba ya Wananchi (
Ukawa), kuhusiana na CCM kuwateulia wananchi viongozi wasio na sifa 
kugombea nafasi mbali mbali.
Alisema, kama kila 
mmoja angetimiza wajibu wake katika nafasi yake hakuna mpinzani ambae 
angechaguliwa ila kuchaguliwa kwa wapinzani ni kushindwa kwa wale
waliowaamini kutoka CCM kushindwa kuwajibika kwa wananchi waliowaamini.
Filikunjombe, 
alisema atakuwa mbunge wa mwisho kunyoshewa kidole na watanzania 
wakiwemo wananchi wake wa Ludewa kwa kushindwa kuwatumikia wananchi na
chama chake cha CCM .
Alisema, hakuomba ubunge kwa ajili ya kujinufaisha binafsi ila aliamua 
kugombea ili kuwatumikia wana Ludewa kwa kuwapelekea maendeleo hivyo k
azi yake kwa sasa hadi mwisho wa ubunge wake ni kuleta maendeleo kwa
wananchi wake na kuona ahadi zake zinatimia kwa muda uliopangwa na si 
kujinufaisha kwa wakati.
"Naomba kwanza mtambue kuwa wabunge wote tulipo fika bungeni kwa mara ya 
kwanza tulikopeshwa sh. milioni 90 kwa ajili ya kununua gari la 
kutembelea na Mimi kwa kuwa nilikuwa na gari pesa hizo niliamua kununua 
gari la wagonjwa Mlangali ambao hawakuwa na gari la wagonjwa
….lengo langu kutumikia wananchi na kuwatatulia kero zao si
vinginevyo”alisema
Akielezea msaada huo wa vitu mbali 
mbali vyenye thamani ya Tsh milioni 40 alivyotoa alisema ni pamoja na
kitanda cha kujifungulia wajawazito chenye thamani ya Tsh milioni 
5.2, Darubini, pesa ya taslimu sh. milioni 1 bati zaidi ya 500, rangi 
debe 20, saruji mifuko 525 na vifaa vingine vingi kwa ajili ya 
kuchangia ujenzi wa miradi mbali mbali ya kijiji na ujenzi wa 
makanisa, shule na wodi ya wazazi.
Awali 
viongozi ukawa wa kijiji cha Mavanga kata ya Mavanga walimpongeza 
mbunge huyo kwa kuwa mbunge wa mfano Ludewa japo wapo viongozi 
wengi ndani ya chama chake ni wabovu.
Mwenyekiti 
wa Ukawa Mavanga John Mligo akishukuru kwa msaada huo wa vifaa na 
fedha toka kwa mbunge Filikunjombe alisema kama wabunge na viongozi wote
wangefanya kama mbunge huyo kamwe wananchi wasingekichukia chama 
hicho.
Akizungumza 
katika mkutano huo mwenyekiti huyo wa Ukawa na mwenyekiti wa serikali 
ya Kijiji cha Mavanga Hilmar Mpambichaka (Chadema), walisema wao
kama viongozi wa upinzani hawana shaka na uwakilishi wa mbunge 
Filikunjombe ndani ya jimbo hilo na nje ya jimbo hilo.
"Tumekuwa na wabunge saba ambao wametangulia kabla ya Filikunjombe ila 
uwakilishi wake umekuwa wa kuigwa na wabunge wengine na kama wabunge 
kote nchini wangekuwa watendaji hivyo huenda upinzani nchini 
usingekuwepo,”alisema Mligo
 
alisema chanzo cha kijiji hicho kuchagua mwenyekiti wa Serikali ya 
kijiji kutoka Chadema ni baada ya viongozi wa CCM kuonyesha kuwa mbali 
na wananchi na baadhi yao kutafuna fedha za michango ya wananchi.
Mligo alisema shida ndani ya CCM ni vita ya wenyewe kwa wenyewe ndio 
ambayo imekuwa ikiwachanganya wananchi na kujikuta wananchi wanaingia 
katika 
mgawanyiko na kuchagua wapinzani.
Alisema 
wakati wa kampeni hata wasio na sifa wanataka kuchaguliwa kwa kutumia 
rushwa, hivyo kutaka kwa Ludewa kutambua wazi mbunge anayekubalika ni 
Filikunjombe pekee na kuwa hawahitaji mtu zaidi ya mbunge wao 
aliyewavusha na kuwafikisha katika maendeleo ya kweli.
Huku 
mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Mpambichaka akiwataka 
wananchi wa Ludewa kuacha kuonja sumu kwa kubadili wabunge na kuwa 
utendaji wa Filikunjombe hakuna wa kumfananisha nae.
Alisema 
kuwa wamepata kushuhudia utendaji wake ndani ya bunge kupitia kamati ya 
PAC kwa kupambana na ufisadi kupitia Escrow na kuwafanya mawaziri zaidi
ya watatu kujiuzulu.
Pia 
kupitia utendaji wake ndani ya jimbo amefanikiwa kuwavuta wana Ludewa 
ambao siku zote walikuwa wakiona aibu kuweka wazi kuwa ni wakazi wa 
Ludewa na badala Yake kudanganya kuwa wao ni wazaliwa wa Mkoa wa Ruvuma
kutokana na awali 
Ludewa kuwa nyuma kwa maendeleo.
"Toka Filikunjombe ameingia madarakani mwaka 2010 na kuwepo kwa kasi ya 
maendeleo ndio tunashuhudia wana Ludewa wakirejea Nyumbani na 
kujitangaza kuwa wao ni wakazi wa Ludewa tofauti na zamani wengi 
walikuwa wakijificha kwa aibu,"
Hata
hivyo alisema wapo wabunge ambao wamekaa majimboni muda mwingi kama 
akina Mzindakaya huko Sumbawanga ila siku zote ni mtu wa kueleza jinsi
alivyofanya Kazi na Mwl Julius Nyerere ila si kujipambanua namna gani 
alivyoleta maendeleo jimboni
Kuhusu 
misaada mbali mbali iliyotolewa na mbunge huyo kijijini hapo mwenyekiti 
huyo alisema kwa mara ya kwanza toka wabunge 7 waliopita kijiji hicho 
kimepata kupata misaada mingi kutoka kwa mbunge huyo.

No comments:

Post a Comment