KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 11 May 2015

TUME KUGAWA MAJIMBO KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU


Mwenyekiti wa Tume, Lubuva

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inatarajia kugawa majimbo ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Tume ya uchagu ndiyo yenye jukumu la kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge kwa mujibu wa Ibara ya 74(6) (c) ya Katiba ya Tanzania ya waka 1977.
Hata hivyo Tume hiyo haikutoa idadi ya majimbo kwa kuwa inategeme kupokea maombi kutoka hatika Halmashauri na kwamba kesho itatoa tangazo kwenye gazeti la serikali na kueleza kila kitu.
Akisoma taarifa kuhusu ugawaji wa majimbo hayo mbele ya viongozi wa vyama vya siasa nchi, jijini Dar es Salaam jana, Kurugenzi wa NEC, Julius Malaba, alisema kwa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi, hivyo tume inatakiwa kuanza maandalizi mapema ili kuweza kufanikisha uchaguzi huo.
Alisema, moja ya maandalizi ambayo yanatakiwa kufanywa na tume hiyo ni kuchunguza mipaka na kugawa majimbo kwa sababu kuna halmashauri mpya zimeanzishwa, na kwa mujibu wa Sensa iliyofanyika 2012, idadi ya watu imeongezeka.
Malaba, alisema katika ugawaji huo tume itakuwa na vigezo maalumu huku ikizingatia mipaka ya kiutawala.
Alisema kwanza mgawanyo huo utazinga wastani wa idadi ya watu katika jimbo inayopatikana kwa kuchukua idadi ya watu wote nchi nzima na kuwagawanywa kwa idadi ya majimbo yaliyopo.
‘Population quota’ itazingatia hali halisi ya idadi ya watu mijini na vijijini.
“Kigezo cha ‘Population quota’ ndicho kigezo kikuu na cha kwanza kitakachotumika katika kuamua majimbo gani yagawanywe,”alisema Malaba.
Kwa mujibu wa makadirio ya Ofisi ya Takwimu mpaka 2015 Watanzania wote kwa upande wa Bara watakuwa wamefikia milioni 47, 110,506.
Kwa upande wa majimbo ya mijini watu milioni 10,069,159 na vijijini ni 37,041,347, hivyo ‘population quota’ kwa upande wa majimbo ya mijini itakuwa ni 325,000 na kwa upande wa majimbo ya vijijini itakuwa ni 235,000.
 Alisema kwa maana hiyo, majimbo yatakayostahili kuwasilisha maombi kwa mujibu wa utaratibu ulioanishwa ni yale tu yenye idadi ya watu zaidi ya idadi ya ‘population quota’.
Idadi ya watu itakayotumika ni ile iliyotokana na makisio ya ongezeko la watu hadi Julai, 2015 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.
Majimbo yenye watu wengi yatafikiriwa kugawanywa.
Malaba alisema takwimu zitakazotumika katika kigezo hiki zitapatikana katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Upatikanaji wa mawasiliano hapa itaangaliwa urahisi wa mwakilishi kuwafikia/kuwasiliana na anaowawakilisha katika maana ya barabara, simu, vyombo vya habari.
Hali ya kijiogrfia, itangalia jimbo liko sehemu gani kwa mfano , maeneo ya mlimani, visiwani au mabondeni kwa lengo la kuona ni kwa jinsi gani litawasilishwa kwa ufanisi.
Alisema kigezo kingine kitakuwa ni uchumi hapa uangalifu utachukuliwa, ili maeneo ambayo yako juu kiuchumi yasimeze kiuwakilishi maeneo yaliyo chini kiuchumi, maeneo yalio chini kiuchumi yatafikiria.
Aliongeza kuwa ukubwa wa eneo la jimbo pia utaangaliwa na maeneo yenye maeneo makubwa yatafikiriwa.
Kingine ni mipaka ya kiutawala ambapo katika kugawa majimbo tume itazingatia mipaka ya kuitawala.
Malaba, alisema pale ambapo mipaka ya utawala itabadilika kabla ya tume kufanya ugawaji wa majimbo, tume itazingatia mabadiliko hayo.
Aidha, alisema jimbo moja lisiwe ndani ya wilaya/halmashauri mbili, kigezo hiki kitazingatiwa ili kuepusha mwakilishi kutumikia wilaya/halmashauri mbili tofauti kwa wakati mmoja.
Alisema pia Kata moja isiwe ndani ya majimbo mawili na mpangilio wa maeneo ya makazi ya watu yaliyopo.
Malaba alisema ugawaji huo pia utazingatia mazingira ya Muungano, kama inavyoeleweka kuwa Tanzania ni nchi ya inayounganisha nchi mbili, kwa hiyo ugawaji wa majimbo utazingatia pia upekee wa mazingira ya Muungano.
Alisema tume itazingatia Uwezo wa Ukumbi wa Bunge, katika kugawa majimbo ni muhimu kwa tume kuzingatia uwezo wa ukumbi wa Bunge ili kuepuka kuzidisha idadi ya wabunge kupita nafasi iliyoko katika ukumbi huo.  

No comments:

Post a Comment