Aliyewahi kuwania jimbo la Arumeru Mashariki kupitia CCM Sioi Sumari akijinadi mbele ya Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha Edward Lowassa
katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo Mh.
Lowassa alikuwa mgeni rasmi.
(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mbunge wa Viti Maalum, Namelock Sokoine akinadaiwa na
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha Edward
Lowassa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo
Mh. Lowassa alikuwa mgeni rasmi.
………………………………
Baadhi ya wagombea waliotangaza nia
kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali mkoani Arusha kupitia CCM juzi
walionekana kupigana vikumbo na wengine wakijinadi mbele ya waziri mkuu
mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani hapa Edward Lowassa.
Lowasa,ambaye anatajwa kuwania urais
kupitia CCM mwaka huu mwishoni mwa wiki iliyopita aliendesha harambee ya
ujenzi wa msikiti wa Patandi uliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha
akimwakilisha makanu wa Rais,Dk Mohammed Billal na kufanikiwa kukusanya
zaidi ya kiasi cha sh,235 milioni ikiwa ni zaidi ya makisio ya msikiti
huo kukusanya sh,200 milioni .
Baadhi ya watia nia wa CCM
walionekana wakichangia fedha katika harambee hiyo huku wengine
wakitumia mwanya wa kunadi sera pindi walipokaribishwa jukwaa kuu.
Wagombea hao watarajiwa wa ubunge ni
Mustapha Panju alitoa Sh6 milioni, Sioi Sumari (Sh7 milioni), Kim Fute
(Sh3 milioni), Philemon Mollel (Sh5 milioni), mbunge Peter
Serukamba (Sh3 milioni) na mjumbe wa NEC kutoka jimbo la Busega, Dk
Raphael Chegeni alichanga Sh1 milioni sawa na mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema na Namelock Sokoine.
Hatahivyo,wakati wagombea hao kwa
nyakati tofauti mara walipofika kuchangia harambee hiyo na kupewa nafasi
ya kusema neno ndipo badhi yao walisikika wakinadi sera kitendo
kilichopelekea kuibua shangwe kwa wahudhuriaji.
Mke wa mtia nia wa CCM,Violet Mfuko
ambaye mmewe ametangaza nia,Kim Fute alifika jukwaa kuu na kumnadi mmewe
kwa kumwambia Lowasa kwamba ametangaza nia na kuwataka makada wa CCM
kumuunga mkono.
“Mheshimiwa waziri mkuu mme wangu
ametangaza nia jimbo la Arusha mjini,mimi ni mke wake nawaomba jamani
mumuunge mkono”alisema Mfuko na kuibua shangwe
Hatahivyo,mtia nia mwingine wa CCM
jimbo la Monduli mkoani Arusha,Sokoine naye alipopanda jukwaani Lowasa
alitumia nafasi hiyo kumnadi kwa kuwataka makada wa CCM kumuombea kwa
Mungu mambo yake yaende vizuri.
“Jamani huyu naye ametangaza nia huko Monduli tumuombee kwa Mungu mambo yake yaende vizuri “alisema Lowasa
Hatahivyo,Sumari,Monaban,Panju na baadhi ya wagombea
wengine walipanda jukwaa kuu na kisha kujitambulisha kabla ya kuchangia
fedha huku wakitamka ya kwamba wanaomba mambo yao yaende vizuri ili
wapitishwe kugombea ndani ya CCM.
No comments:
Post a Comment