KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 18 May 2015

WANAHABARI WAJENGEWA UWEZO NA PPRA



2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Fedha  za Nje Bi. Doroth Mwanyika akifugua Semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma PPRA katika kuelekea kuadhimisha miaka 10 ya (PPRA)  tangu kuanzaishwa kwake inayofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, Semina hiyo inakutanishwa wawakilishi wa Press Club za kutoka mikoa mbalimbali pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali jijini Dar es salaam ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii, Maadhimisho yameanza leo mei 18/2015 na yataendelea mpaka kilele chake  Mei 20/2015.
1 
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya PPRA Balozi Martin Lumbanga akizungumza katika semina  wakati akitoa salamu zake kwa wajumbe wa semina hiyo.
3
Baadhi ya wakuu wa vitengo na maofisa wa PPRA wakiwa katika semina hiyo inayofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
4
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa PPRA wakiwa katika semina hiyo.
5
Wanahabari kutoka mikoa mbalimbali wakihudhuria semina hiyo.
6 7 8
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika, amesema sio kweli kama sheria ya manunuzi haifai kama baadhi ya watu wanavyojaribu kuuaminisha umma.
Dorothy, alitoa kauli hiyo, wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Elimu ya Manunuzi ya Umma kwa wadau wa habari nchini, iliyoandaliwa na Mamlaka ya Manunuzi (PPRA), iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Alisema, kuwa wahusika wakuu katika manunuzi wakizingatia  sheria hiyo pamoja na kuweka uzalendo mbele, anaamini hata utekelezaji wake utakuwa mwepesi ambao utalisaidia taifa katika kudhibi matumizi yanayokwenda kinyume na sheria hiyo ya manunuzi.
Alisema, kuwamekuwa na malalamiko mengi katika eneo hilo la usimamizi wa manunuzi ya umma, chanzo cha malalamiko hayo yanatotokana uelewa mdogo juu ya sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na Kanuni zake za mwaka 2013, ambazo ndizo hutumika kama mwongozo kwenye manunuzi ya ummma.
“Baadhi ya watu wanadiriki kusema kuwa sheria hii haifai kwa kuwa inachangia kuongeza gharama pamoja na muda wa kufanya manunuzi serikalini,”alisema Dorothy.
Alisema, huo ni utetezi tu, lakini ukweli ni kwamba Sheria hiyo na kanuni zake kiujumla zimeweza kiasi fulani kuziba mianya ya ufujaji wa fedha iliyokuwa ikitumiwa hapo awali na baadhi ya watu wasiokuwa waadilifu kwa Watanzania wenzao wakiwemo watumishi wa umma na watu binafsi.
Dorothy, aliongeza kwa kusema kuwa utekelezaji fasaha wa sheria hiyo unahitaji manunuzi kufanyika katika mazingira ya uadilifu, uwazi, haki na ushindani mkubwa ili kuhakikisha upatikanaji wa thamani bora ya fedha za umma zinavyotumika.
Akizungumzia wrsha hiyo ya wanahabari, Dorothy, alisema kuwakutanisha wadau wote wabari nchini, anaamini kuwa uamuzi huo umefanywa ili kutii Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ya miaka kumi ya PPRA, inayosema ‘Miaka kumi ya PPRA: Tumethubutu, Tumeweza, Tuendelee kushirikiana kuboresha zaidi manunuzi ya umma.
Alisema lengo la kuandaa warsha, hiyo ni kuwajengea uwezo zaidi wandishi na wadau wa habari juu ya manunuzi ya umma pamoja na sheria na kanuni zinazoongoza sekta hiyo.
Dorothy, alisema kubwa zaidi ni kukumbushana juu ya umuhimu wenu katika kutoa elimu sahihi ya masuala ya manunuzi ya umma na hasa Sheria ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na Kanuni zake za mwaka 2013.

No comments:

Post a Comment