KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday, 7 June 2015

UKAWA TOWENI FURSA KWA MAKADA WANAOTAKA KUTANGAZA NIA ILI WANANCHI WA WAPIME

BAADHI ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wameutaka Umoja wa Katiba ya Wananchi  (Ukawa), kuwapa nafasi ya makada wake wanaotaka kutangaza nia ya kuomba uteuzi wa kuwania nafasi ya urais kupitia umoja huo ili wananchi wawatambue mapema.
Walisema hivyo, kwa vile wanaamini kuwa utaratibu huo ambao unafanyika ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), unaonesha kuwa ni wa kidemokrasia na unazingatia matakwa ya kila mwanachama.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam leo, walisema kukaa kumya kwa umoja huo kunawajengea wasiwasi baadhi ya wanachama kwamba huenda umoja huo umeshindwa kufikia muafaka katika malengo yao.
Mohamed Gema, Mkazi wa Manzese, alisema baada ya watia nia wa CCM kujitokeza imewasaidia kujua ukweli wa kila mmoja katika kuzitambua kero za wananchi na uwezo wao wa kuzitatua uko uje.
“Kiukweli inaonekana wote wanazitambua kero zinazowakabili wananchi lakini hawaoneshi mikakati ya kuzimaliza pindi watakapoingia madarakani,”alisema Gema.
Alisema kutokana na mazingira hayo wanaamini kuna ulazima wa kuwajua watia wa umoja huo ili wananchi wa wajue nao wanazijuaje kero za wananchi na kwamba wanamikakati gani ambayo itasaidia kuwakomboa wananchi katika lindi la umasikini.
“Nchi hii inataka kiongozi amabye anazitambua kero za na agenda za wananchi na sio watu ambao ukiwaangalia tu sura zao hazioneshi kabisa kuguswa na matatizo ya wananchi bali wanalenga masilahi yao pindi watakapoingia Ikulu,”alisema Gema.
Estera Bwire, alisema wanautaka Ukawa kufanya hivyo haraka kwani wamechoshwa kutaniwa na watani zao kuwa hawana mgombea na kwamba wanasubiri makapi kutoka CCM.
Alisema utaratibu wa kuwapata wagombea katika Ukawa hauna tofauti na ule wa CCM hivyo ingekuwa ni vema wakajitokeza tukawajua wanaotaka urais kwa ajili ya kuwapima uwezo wao.

“Wagombea wajitokeze na baadae wakae kwenye vikao vya ngazi ya juu kwa ajili ya kumteua mmoja ambaye atakuwa chaguo la umoja huo, ambaye atapambana na yule wa CCM na vyama vingine,”alisema Ester.  

No comments:

Post a Comment