MBUNGE wa Bumbuli, January
Makamba anatarajia kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na Chama chake
Cha Mapinduzi (CCM), kuwa Mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi
unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Sherehe hiyo ya kutangaza
itafanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
jana, Makamba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
alisema baada ya kutangaza nia anatarajia kuchukua fumu urais mjini Dodoma
Jumanne ijayo.
Alisema katika kutangaza ni yake
hiyo ataelezea mambo mbalimbali yanayogusa maisha ya wananchi kila siku.
Falisafa hiyo itamfanya
awe na uwezo wa kupambana na changamoto za mahitaji ya ulimwengu wa leo wa
kidigitali na siyo analogia ambao walioona “jana nyingi” katika hali yoyote
hawawezi kuzimudu.
Mbali na Profesa Mwandosya,
Wassira, Makongoro na Amina, orodha ya mwaka huu ina majina mengine kama la
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal;
Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo Kayanza Pinda;
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick
Sumaye na Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa.
Wengine waliomo katika orodha
hiyo ni mawaziri ambao ni pamoja na Benard Membe (Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa), Samwel Sitta (Uchukuzi), Dk. Titus Kamani (Mifugo na Uvuvi) na
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.
Wamo pia Naibu Waziri wa Fedha,
Mwigulu Nchemba; Mbunge wa Kuteuliwa, Profesa Sospeter Muhongo; Mbunge wa
Nzega, Dk. Khamis Kigwangala; Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja; Mbunge wa
Kisesa, Luhaga Mpina na kadhalika.

No comments:
Post a Comment