Wafanyabiashara hao walisema hivyo baada ya kudai kuwa wiki tatu zilizopita walivunjiwa meza zo na polisi wakishirikiana na mgambo wa jiji majira ya saa 4:00 usiku bila kuelezwa.
Kitendo hicho kiliwafanya siku iliyofuata wafunge makutano ya barabara za Kawawa na Uhuru kutwa nzima, hali iliyozorotesha shughuli zote uzalishaji katikati ya jiji hilo.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini jana, Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara Walemavu Dar es Salaam (Uwawada), Mohamed Kidumke, alisema kuwa usumbufu wanaopata katika kufidiwa kunatokana na serikali kutojali haki za watu haokwa muda mrefu sasa.
Alisema, hivyo baada ya kubaini kuwa pamoja na kupeleka idadi ya orodha ya wafanyabiashara hao wiki mbilizilizopita inashangaza kuwa maofisa kutoka wilayani kuendelea kuwazunguusha kwa madai kuwa haijakamilika hivyo wanahitaji ifanyike tathimini nyingine.
“Unajua kitengo cha manispaa kinachoshughulikia walemavu hakina ushirikiano mzuri na walemavu na ndio maana pamoja na kufika katika eneo hilo wakati walemavu hao wanakabidhiwa bado hawajui idadi halisi,”alisema Kidumke.
Kidumke, alisema kama wangekuwa wanajali haki za watu hao anaamini wangejua idadi ya watu hao kwa vile wakati wanakabidhiwa eneo waliko vunjiwa meza zao ilitajwa idadi yao.
“Tunatoa siku 15, endapo siku hizo zitapita bila ya kupatikana muafaka basi wanatarajia kuchukua hatua wanazozijua wenyewe.
Aliongeza kwa kusema kuwa kutokana na kuzuunguushwa huko katika kulipwa fidia, wanachama wa umoja huo kwa pamoja wamefikia uwamuzi wakutoa siku hizo 15 kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa kulipwa fidia ya uhalibifu wa meza zao huku wakijiaandaa kwa hatua yeyote ile itakayoamuliwa hapo baadae.
No comments:
Post a Comment