ASKARI wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), jijini Arusha,
PC Raphael Paul (25), amepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha kwa kosa
la kumbaka mwanafunzi wa kidato cha sita Shule ya Sekondari ya Wasichana
Korogwe.
Alisomewa mashtaka hayo jana mbele ya Hakimu Jasmine
Abdul na Wakili wa Serikali, Sabina Silayo aliyedai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa
huyo alitenda kosa Januari 16 mwaka huu eneo la FFU kwa Morombo, jijini hapa na
kumsababishia maumivu ya mwili.
Mwanasheria wa serikali alidai mahakamani hapo kwamba upelelezi
wa shauri hilo umekamilika, Hakimu Abdul aliahirisha kesi hadi Januari 25 mshtakiwa
huyo atakaposomewa maelezo ya awali.
Hata hivyo, Paul alikana shtaka hilo na kupelekwa
mahabusu kwa kuwa kosa linalomkabili halina dhamana.
No comments:
Post a Comment