KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday, 20 January 2016

SERIKALI YATOA SHILINGI MILIONI 7 KWA WATOTO WALEMAVU



SERIKALI imeipatia Sh. Milioni saba Shule ya Msingi Kongowe kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu.
Fedha hizo ni za huduma mbalimbali kwa wanafunzi hao ikiwa ni pamoja na chakula kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Akizungumza jana Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Beatus Lingumbuka, alisema wamepokea kiasi hicho kwa ajili ya matumizi ya shule hiyo ya msingi na aliahidi taarifa za matumizi atawasilisha kwa viongozi wa halmashauri.
Wakichangia kuhusu uboreshwaji wa shule hiyo, Hamza Duluge, aliomba wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo kuchangia baadhi ya mahitaji kwa ajili ya uboreshwaji.
Alisema pamoja na serikali kutangaza elimu bure lakini changamoto haziwezi kumalizika endapo wazazi hawatashikamana na kusaidia baadhi ya mambo kwa makubaliano.

No comments:

Post a Comment