KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday, 28 January 2016

ESTER BULAYA ACHARUKA BUNGENI

MBUNGE wa Bunda Ester Bulaya leo, aligeuka kuwa mwiba kwa wabunge wa CCM kwa kuwataka wawe watu watulivu pale wabunge wengine wanapokuwa wakichangia bungeni.
Hali hiyo ilijitokeza jana bungeni ambapo Bulaya alikuwa akiuliza swali la nyongeza huku wabunge wa CCM wakipiga kelele jambo ambalo lilimkera Bullaya na kuwataka wakome.
Bullaya ambaye alikuwa mbunge wa Viti Maalum 2010-15 kwa tiketi ya CCM na sasa ni mbunge wa Jimbo la Bunga (Chadema) kwa kumgaragaza mkongwe wa Siasa,Steven Wasira.
Bila kuwaonea aibu wabunge wa CCM Bullaya aliwataka wa chama tawala kuwa watulivu na wenye kusikiliza pindi wawapo katika shughuli za bunge badala ya kuwa na tabia ya kuzomea zomea.
Bullaya alilazimika kuwakemea wabunge wa CCM pale alipokuwa akiuliza swali la nyongeza huku wabunge wa chama tawala wakionesha kupiga kelele zilizokuwa zikiashiria kuondosha utulivu ndani ya ukumbi wa bunge.
“Komeni” ni kauli ambayo aliitoa Bullaya alipokuwa akiuliza swali la nyongeza hata hivyo kauli hiyo ilionekana kuwa na nguvu kubwa ndani ya ukumbi wa bunge kutokana na wabunge wote kuufyata na kuwepo kwa utulivu mkubwa ndani ya kukumbi wa bunge tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali.
Katika swali la nyongeza la mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kutoa fidia kwa wananchi wa vijiji mbalimbali vya jimbo la Bunda ambao wanashambuliwa na tembo huku hakuna wananchi hao hawalipwi fidia.
Mbunge huyo alitaka serikali iweke wazi ni lini itakuwa na ufumbuzi wa kudumu wa kuweka ulinzi katika mipaka ili kuwazuia tembo ambao uvuka mipaka kwa lengo la kushambulia mazao ya wananchi na wakati mwingine kusababisha vifo kwa wananchi.
Awali katika swali la nyongeza la mbunge wa Serengeti,Marwa Chacha (Chadema) alitaka serikali ieleze kama tembo anathamani kuliko mwanadamu.
Mbunge huyo aliuliza swali hilo kutokana na adhabu ambayo utolewa kwa yule ambaye anabainika kuuwa tembo kwa kutozwa faini kiasi cha sh.milioni 25 huku tembo akimuua mtu ulipwa kifuta jasho cha sh.milioni 1 tu.
Wakati huo huo vijembe vya chini chini vilisikika wakati wa kipindi cha kuwaapisha wabunge wapya na mawaziri ambao walianza kazi bila kuapishwa.
Mapema kabla ya kuendelea na shughuli za Bunge kwa maana ya kipindi cha maswali na majibu Spika wa Bunge Job Ndugai aliwaapisha wabunge 9 wapya kati yao watatu wakiwa katika baraza la mawaziri.
Wakati Spika akiendela kuapisha wabunge hao vijembe vilisikika vikitolewa na wabunge wanawake wa CCM wakidai 8 kwa moja wakiwa na maana walioapishwa ni tisa kati ya hao ni mmoja tu wa upinzani na waliobaki ni kutoka CCM.
Walioapishwa ni ,Dk.Abdallah Possi (kuteuliwa),mbunge wa Ludewa Deogratias Ngalawa (CCM),mbunge wa Arusha mjini,Godbless Lema(Chadema),mbunge wa Ulanga magharibi,Googluck Mlinga (CCM),mbunge wa Kuteuliwa Prof.Makame Mnyaa Mbarawa (CCM),mbunge wa Handeni, Omari Kigoda (CCM),mbunge wa Kuteuliwa Dk.Philip Mpango(CCM),mbunge wa Masasi Rashid Chuachua (CCM) na mbunge wa Lushoto Shabani Shekilindi(CCM).

No comments:

Post a Comment