KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday, 3 February 2016

KANDA YAONGOZA KWA MAAMBUKIZO YA MAGONJWAYALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE (NTDs)

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesema Kanda ya Ziwa inaongoza kwa maambukizo ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTDs).
Miongoni mwa magonjwa hayo ni Usubi, Trakoma, Kichocho, Minyoo, Mabusha na Matende.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa magonjwa hayo kutoka wizara hiyo, Dk. Upendo Mwingira, alisema kuwa serikali inaanza kampeni leo ya kutoa dawa ya kujikinga  na ugonjwa wa kichocho kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema kila baada ya mwaka mmoja wanatoa dawa kwa watoto ya  kujikinga na ugonjwa huo inayoitwa Prazi Quantel.
Mwingira alisema kabla ya kupewa dawa hizo watoto lazima wapewe chakula  na wakae muda wa saa mbili kisha wapatiwe dawa hizo.
“Ugonjwa wa kichocho huenezwa kupitia konokono na unasababishwa na minyoo ambayo inaishi katika maji yaliyotuama na binadamu hupata maambukizo ya ugonjwa huo mara baada ya kuogelea katika maji yaliyotuama, alisema.

Alisema Tanzania iliridhia kudhibiti ugonjwa huo kufikia mwaka 2020 na kazi hiyo inajikita zaidi kwenye umri hatarishi ambao ni watoto wenye umri wa kwenda shule.

No comments:

Post a Comment