KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday, 3 February 2016


P.O.Box 12349, Dar es Salaam,  Mbezi Beach Park, New Bagamoyo  Rd
 Tel: +255 755 953 946, 755 395 517, E-mail:  .f 11  r '',c     iit111'1Ct.






TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI




Chama Cha   Kijamii  (CCK)  kimemsimamisha  kazi mara  mojo  Naibu  Katibu  Mkuu wake wa  Zanzibar  Ali K hatib Ali, ambaye pia  alikuwa mgombea nafasi  yo Urais wa Zanzibar   kwenye uchaguzi uliotangazwa kufutwa no  Tume  yo  Uchaguzi  Zanzibar ( ZEC) Oktoba 2015.
Pamoja na kusimamishwa uongozi, Ali K hatib Ali pia amesimamishwa uanachama wake ili kupisha  uchunguzi  dhidi  yoke   kufuatia   uamuzi wake  binaf si   wa   jana kuutangazia umma kuwa CCK  itashiriki  uchaguzi wa  marudio huko  Zanzibar uliotangazwa no ZEC kurejewa Machi 20, 2016.

ldara yetu yo  Ulinzi na  Usalama wa  chama iliyo  chini  ya Mwenyekiti wa  Taifa, jana ilitupatia  taarifa za kuwepo mpango wa  siri wa  Naibu Katibu Mkuu huyu, kurotibu kikao na  waandishi wa  habari huko  Unguja no baadae kufanikiwa kunasa taarifa za kikao  hicho kilichorushwa moja kwa  moja na  kituo kimoja cha Radio visiwani  humo.
Ndipo  uamuzi wa    kuitishwa  kikao   cha  dharura  cha  sekretarieti leo   asubuhi ukafanyika, lengo likiwa  ni  kujadili no  kutoa uamuzi juu  ya  tamko hilo  Ia  ndg.  Ali Khatib Ali.
Baada majadiliano  ya  takribani   masaa   mawili    kikao    kwa    kauli    moja kimekubaliana   kumsimamisha kazi  pamoja   na   uanachama  ndg. Ali  Khatib  Aii baada yo kujiridhisha kuwa amejipa mamlaka ya  kutoa tamko kinyume cha katiba yo CCK kifungu cha 16.2 (a) . kwa  jambo zito kama hilo.

Ndg. Ali K hatib Ali amebainika kukiuka wajibu wake kikatiba kama kiongozi chini  ya kifungu 7.3  (b)  na  kwamba  Sekretarieti kutilia  mashaka kuwepo kwa  mazingira  ya rushwa kufuatia hatua hiyo yoke  kutangaza tamko hilo.

Hivyo  CCK  kimekubaliana pamoja  na  mambo mengine kuunda kamati ndogo yo kumchuhguza yenye wajumbe wanne itakayoongozwa na  Mwenyekiti wa  Mkoa wa    Shinyanga   na   Mkurugenzi  wa    Ulinzi  na    Usalama,  Masamalo  Masamalo, Onesphor Nchimbi, Rukia  Abdi na  Ali Waziri Gombati na kutakiwa kukamilisha  kazi hiyo  katika muda mf upi no ripoti kupelekwa Kamati Kuu wiki ijayo.
Aidha CCK  inasisitiza  kuwa suluhu  ya  mgogoro wa  Zanzibar  siyo ujanja ujanja bali kuheshimu taratibu na sheria  zilizoko, aidha chama chetu kinaona kwa hali  ilivyo  si sahihi   hata  kidogo  kwa ZEC  kuitisha    uchaguzi  tulipashwa  kuelezwa  na   ZEC kilichotokea badala ya kulazimisha mambo kibabe.


No comments:

Post a Comment