UCHAGUZI WA MEYA WA JIJI WAAHIRISHWA KWA AMRI YA MAHAKA, POLISI WAPAMBANA NA MADIWANI WA UKAWA
Mbunge wa Kibamba John Mnyika akiongea na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe kupata ufumbuzi baada ya uchaguzi kuahirishwa kwa amri ya mahakama.
……………………………………………………………………………………………………………
VURUGU
kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, mara baada
ya uchaguzi huo kuairishwa tena mwa mara ya tatu
leo.
Baada ya kutokea vurugu hizo, Jeshi la Polisi lilivamia ukumbi wa Karimjee na kwa ajili ya kutuliza
ghasia zilizotokea baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi.
Uchaguzi huo umeahirishwa baada ya kufunguliwa kesi Mahakamani hata hivyo, Madiwani na wabunge waUmoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Tukio
hilo la aina yake limetokea muda huu Jijini mara baada ya Mkurugenzi wa
Jiji kutangaza kuahirishwa kwa uchaguzi huo kwa madai ya kusimamishwa
na mahakamani, huku jambo hilo lilowachukiza madiwani wa Ukawa
wakidai kuwa hawajapata barua hiyo ya kesi hiyo.
Mara baada ya Ukawa kugomea
hoja hiyo ndipo wakafikia hatua ya kutaka kufanya uchaguzi
wenyewe, wakidai kuwa akidi ilikuwa imetimia kwa ajili uchaguzi huo.
Kutokana na madai yao hayo, wakaomba
waendelee kufanya uchaguzi huo, jambo lililochukuliwa kuwa wanakaidi amri halali ya
mahakama ya kusimamisha uchaguzi huo kutokana na kesi ya msingi iliyoko mahakamani.
Wakati
wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo Ukawa wenyewe, ndipo Polisi zaidi ya 15
wakaingia ukumbini humo na kuwataka madiwani hao
waachane na zoezi hilo na kuondoka ukumbini.
Kitendo hicho kiliwachukiza
madiwani hao na kuanza vurugu hali iliyowafanya Polisi kuanza kupambana na
madiwani hao wa Ukawa ili kuwatoa nje.
No comments:
Post a Comment