KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Saturday, 27 February 2016

SHINDANO LA KUIBUA VIPAJI LA THE AFRICAN MASTER MIND AWARD KUZINDULIWA KESHO MKOANI MBEYA



TAASISI ya Dream Success Interprises inatarajia kuzindua shindano linalojulikana kwa jina la 'The African Master Mind Award', ambapo mshindi wa jumla atajinyakulia tuzo yenye thamani ya sh. milioni 5, Octoba mwaka huu, uzinduzi huo utakaofanyika kesho mkoani Mbeya.
 Hilo ni Shindano la tatu tangu taasisi hiyo ilipoanzisha shindano hilo mwaka 2014 ambako washiriki walipatiwa tuzo miongoni mwao alikuwemo aliyewahi kuwa CAG,
Ludovick Utouh, Vick Mtetema na Saed Kubenea.
 Akizungumza na mwandishi, Ofisa Mtendaji wa Tasisi hiyo, Charles Makoba, alisema shindano hilo linalengo la kuibua na kuwatunuku wale wote waliyoonesha uadilifu katika kulitumikia Taifa.
Alisema lengo la Shindano hilo, ni kuibua fikra mbadala zitakazochangia kumaliza tatizo la ajira nchini na barani Afrika kwa ujumla na kuunganisha vijana wa bara hilo ili waweze kuwa na sauti moja katika kupigania masilahi katika bara hilo. 
Aidha, Makoma, alisema washiriki wote watakaoshiriki shindano hilo wtatoa hotuba fupi ya muda wa dakika kumi kwa kila mmoja. 
Akizungumzia uzinduzi huo, Mkurugezi wa Mipango wa taasisi hiyo, Joshua Laurence, alisema maandalizi yamekamilika na washiriki wote wako tayari kwaajili kesho.
 "Tukimaliza hapa Mbeya uzinduzi utaendelea katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Arusha, "alisema Laurence ambaye yuko mkoani Mbeya.
Alisema uzinduzi katika mikoa hiyo unalenga kupata washiriki 10 ambao wataingia katika hatua za mwisho za kumpata mshindi wa Taifa kwa ujumla ifikapo Okotoba mwaka ambapo siku hiyo itakuwa Ile ya Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa hayati Julius  Nyerere.
 "Shindano hili pia litaboresha uchumi wa Watanzania kwa kuwaanzisha kampuni za fani mbalimbali walizosomea ikiwemo ujuzi unaotokana na vipaji na hiyo itakuwa ni moja ya msaada wa utekelezaji wa hotuba ya Rais John Magufuli, "alisema Laurence.
 Lawrence, aliwataja waandaji wazalishaji wa virutubisho lishe vya Tangreen Juice na Blue Juice.

No comments:

Post a Comment