Umoja wa Wafanyabiashara wa Mifugo na Mazao yake Vingunguti
(Uwamivi Society),katika machinjio
ya Vingunguti, wilayani Ilala, wamemtaka Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi, Mwigulu Nchemba kuingilia kati
mgogoro wa ndani ya umoja huo, ambao unaikosesha serikali mapato.
Baadhi ya wanachama wamefichua siri ya machinjio hiyo ya ukusanyaji
wa mapato kidogo ukilinganisha na mifugo inayoingizwa manjioni hapo kuwa kumechangiwa
na mfumo mbovu unaolelewa na Mkurugenzi, wa wilaya hiyo, Isaya Mngurumi.
Hayo yalifichuliwa jijini Dar es Salaam juzi, wakati
wafanyabiashara wa machinjio hiyo walipozungumza na wandishi wa habari kuhusu matumizi mabaya ya fedha za miradi huo, yanayofanywa
na uongozi wa Uwamivi.
Akielezea sakata hilo, Prasidus Mbita alisema viongozi wa
umojaa huo wametungwa sheria za kuhakikisha kila mfanyabiashara anaingiza
ng'ombe wawili hata kama ana uwezo wa kuingiza zaidi ya hao.
"Pindi wafanyabiashara wanapozidisha mifugo zaidi ya
hiyo vingozi wa umoja huo unakusanya sh. 10,000 kwa kila ng’ombe mmoja aliyezidi
huku fedha hizo zikiingia mifukoni mwao hali inayoikosesha serikali mapato.
"Utaratibu huo wa kulazimisha wafabiashara kuchinja
ng'ombe wawili wakati mwingine pia kunasababisha upungufu wa nyama sokoni hivyo
kufanya bei ya nyama kupanda," alisema Mbita.
Mbita, alisema kutokana ubadhirifu huo ulisababisha baadhi ya
waliokuwa wanachama wa umoja huo wanaofikia 55 kujitoa na kumuandikia
malalamiko kwa Mkurugenzi ili kumfahamisha namna mapato ya serikali yanavyohujumiwa
na majipu.
"Lakini cha kusikitisha baada ya kutuma barua hiyo
Mkurugenzi alitoa jibu la kutukatisha tamaa kwa kututaka wafanyabiashara wote
kukubali kuchangia umoja huo," alisema Mbita.
Akizungumza sababu za wao kujitoa kwenye umoja huo, Mailo
Machage alisema pamoja na kuwa ndani ya umoja huo kwa miaka mitano
wakichangishwa fedha za mauzo ya damu ya wanyama hata hivyo, hawaoni kwa namna
gani watanufaika na umoja huo.
"Kwa siku tunachangia pipa 20 zenye thamani ya sh.
600,000 lakini tunapohoji mapato na matumizi eti tunaambiwa fedha zitakazopatikana
zitapelekwa kwa watoto yatima," alisema Machage.
Naye Othman Kailo aliongeza kuwa hata baada ya kujitoa umoja
huo umeendelea kuwatoza michango na hata walipotaka kurudishiwa michango
waliyochangia walikataliwa.
Alipotafutwa Mwenyekiti wa umoja huo Anatolio Lubeleje
alikana kuwepo kwa madai hayo na kusema kwamba kila mwaka wamekuwa wakifanya
mikutano na kusoma mapato na matumizi.
Akijibu malalamiko hayo Mkurugenzi wa Manispaa ya
Ilala, Isaya Mngurumi, aliwashauri wanachama hao kuwa kama wanahisi wanafanyiwa
mambo kinyume na katiba wajitoe katika chama hicho na kuunda umoja wao ambapo
manispaa itashirikiana nao kwa kuwapa viongozi wa kuwasimamia.
Alisema wakati mgogoro huo unachipua alikutana na uongozi na wadau hao kwa pamoja wakakubaliana kila mfanyabaishara atachinja ng’ombe kulingana na orodha ya wateja wake na sio vinginevyo.
Alisema wakati mgogoro huo unachipua alikutana na uongozi na wadau hao kwa pamoja wakakubaliana kila mfanyabaishara atachinja ng’ombe kulingana na orodha ya wateja wake na sio vinginevyo.
“Kama leo wanalazimishwa kuchinja ng’ombe wawili hilo ni
kosa na haliko katika katiba yao, kwa sababu kama mahitaji ya nyama ni makubwa
kwa nini wapangiwe kiasi cha kuzalisha bidhaa? Nawashauri watafute katiba ya
chama chao waisome kwa makini watafute ufumbuzi haraka bila hivyo watakatana
mapanga,” alisema Mngurumi.
Alifafanua kwamba chama hicho kimesajiliwa na serikali
Septemba 2012, kwa nembo ya picha ya Ng’ombe, Mbuzi , Kondoo na Ngozi.
No comments:
Post a Comment