KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 29 February 2016

MAFUNDI MAGEREJI WAAPA KUFA KWENYE ENEO WANAKOFANYIA KAZI


UMOJA wa Mafundi Magari wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wameapa kutoondoka katika eneo wanalofanyia kazi kwa madai ya kumpisha mtu aliyetajwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kuwa ni muwekezaji wa eneo hilo.
Kauli hiyo inakuja siku chache baada ya Kaimu Kamishna wa Ardhi, Makondo kuwataka kuondoka katika eneo hilo kwa masharti ya kugawana eneo hilo la hekar 32 nusu kwa nusu.
Akizungumza kwenye mkutano ambao walitarajia kukutana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob, ambaye hata hivyo hakutokea kutokana na kutingwa na majumu mengine, Naibu Katibu wa Umoja huo, Gratia Mbelwa, ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Madale kupitia (CCM), alisema kinachofanywa na wizara hiyo ni kiini macho ambacho hawako tayari kukikubali.
Alisema agizo la wizara wizara hakitekelezeki kwa vile utaratibu wa kufikia maamuzi hayo ulikuwa wakibabe ambao umetolewa zaidi kwa kujali masilahi ya mtu huyo ambaye hawamfamu tangu kuanza kwa mgogoro huo kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Mbelwa, alisema wameshangazwa na barua ya Kamishna huyo wa Ardhi kwa kudai kuwa ili kumaliza mgogoro huo ni lazima pande mbili zinazovutana kubaliana na uamuzi uliyofikiwa katika mazungumzo kati yao kwa pamoja.
Aliyataja mapendekezo hayo kuwa ni muwekezaji aliyetajwa kwa jina la Nyanza Roads Works aachie ekari 16 kutoka kwenye eneo hilo lao wanalomiliki kisheria.
Vilevile umoja wa Mafundi hao waondoe miundombinu yao iliyoko katika eneo hilo na kuipeleka kwenye eneo la ekeri 16 watakaotengewa.
Kingine kilichoanishwa kwenye barua hiyo, ni Wizara ya Ardhi kwa kushirikiana na  Manispaa ya Kinondoni wamege ekari hizo 16 kisha kuzipima, kuonesha na kuwamilikisha umoja huo wa mafundi magari (Tegeta Magereji).
Pia Kamishna huyo katika barua hiyo amemtaka Nyanza Roads Works kurejesha Hata halisi (CT.NO.29971) kwa Kamishna wa Ardhi ili zoezi tajwa hapo juu liweze kukamilika.
“Tunataka kuifahamisha Wizara ya Ardhi, kuwa hawako tayari kuondoka kwa masharti hayo kwani wakati uwamuzi huo baadala yake tunamtaka waziri wa wizara hiyo Wiliam Lukuvi kutembelea eneo hilo na kujionea hali halisi kama kweli hicho kinachodaiwa kinawezekana,”alisema Mbelwa.
Alisema, kuwa Wizara inapaswa kuheshimu uwamuzi wa Manispaa ya Kinondoni ambayo inaamini kuwa eneo hilo ni la mafundi kutokana na makubaliano ya awali wakati wanakabidhiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Yusuf Makamba.
Awali, Mwenyekiti wa Umoja huo, Alawi Kassimu, alipokuwa akiwasome maagizo hayo ambayo alidai kuwa wakati walipokutna na Kamishna huyo walitakiwa kubali mapendekezo hayo bila ya kutoa hoja.
Hata hivyo baada ya kuisoma barua hiyo mafundi walichangia mapendekezo hayo kwa muunkari ya juu wakipinga agizo hilo.
Kitendo hicho kilimfanya mwenyekiti huyo kuwataka mafundi wenzake kupunguza jazba wakati wanapojadili suala hilo kwani kunaweza kuwafanya waonekane wakorifi na kukosa haki yao.

No comments:

Post a Comment