KIKAO cha Bodi ya Barabara zilizo chini ya Wakala wa Barabara Tanzania
(Tanroads), kimeingia dosari baada ya wabunge sita wanaotoka vyama vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kususuia kuhu ,mbunge wa Kinondoni Maulid
Mtulia, akihudhuria.
Wabunge waliosusia kikao hicho ni
Abdallah Mtolea, Said Kubenea, John Mnyika, Anatropia Theopist na Halima Mdee,
Mwita Waitara ambao walipandishwa kizimbani.
Alipotawa Mtulia kufahamu mbona amehudhuria kikao hicho huku msimamo wa
Umoja wao ukiwa ni kususia ambapo alisema, ushiriki wake katika kikao hicho
haikuwa makusudio yake bali kulichangiwa na mawasiliano dhaifu baina yake na
wenzake.
“Unajua suala hili linagusa sehemu tatu kwanza kuna upande wa wananchi
waliyonichagua, kuna masilahi ya chama na huu umoja wetu, sasa ningeapewa
taarifa hata hivyo ingebidi tujadiliane kabla ya kuchukua uamuzi,”alisema
Mtulia.
Alisema hata juzi wakati wenzake wanasusia ziara ya kutembelea miradi yeye
hakwenda lakini siyo kwasababu ya ya msimamo wa Ukawa bali kwakuwa hakuwepo na
hakuwa na taarifa hiyo.
Hata hivyo, Mtulia alisema kama angepata
taarifa mapema asingeshiriki na kwamba kilichotokea ni bahati mbaya, baada ya
kumaliza kuzungumza na wandishi wa habari alitoweka katika Kikao hicho.
Hata hivyo, kuhudhuria kwa Mtulia kulisababisha akidi ya wajumbe kutimia
kwani walifika saba kati ya 12 hivyo kumchangua Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Aliyeshinda nafasi hiyo ni mbunge wa Ilala, Mussa Zungu, baada ya jina lake kupendekezwa
na Mbunge wa Kigamboni Faustin Ndugulile, kisha kupitishwa na Wabunge hao
wachache wa mkoa wa Dar es Salaam
wa CCM.
Ukawa juzi wakati wakisusia ziara ya kutembelea miradi ya barabara jijini
walisema hakuna haja ya kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na
uhasama uliyojitokeza hususani baada ya tukio la kuahirishwa uchaguzi wa Meya
Februari 27, mwaka huu.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Saidi Meck
Sadik, amesema Mkoa huo umetengewa zaidi ya sh. bilioni 343 kwa ajili ya ya
mipango ya matengenezo ya barabara katika kipindi cha mwaka wa fedha wa
2016/2017.
Akizungumza kwenye Kikao hicho, Sadiki,
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, alisema lengo kuu la bodi ya barabara ya
mkoa ni kuratibu, kushauri na kufuatilia maendeleo ya miundombinu ya barabara
katika mkoa huo.
Alisema kuwa kuna haja ya watendaji
wote kujiepusha na matumizi ya fedha hizo na kwamba kila takayekwenda kinyume
na matumizi ya fedha hizo hatavumiliwa na hatua kali dhidi yake zitachukuliwa.
“Ni matumaini yangu kuwa kiasi hiki cha
fedha kitatumika kama ilivyokusudiwa ili
kupata thamani halisi ya fedha hizo, matumizi thabiti ya fedha hizo zitasaidia
kwa kiasi kikubwa kukabiliana na baadhi ya matatizo yaliyopo ya miundombinu ya
barabara za mkoa wetu,”alisema Sadik.
Sadik, alisema anatahadharisha hivyo,
kwa vile kumekuwepo na baadhi ya mamlaka ambazo hazipendi kuzingatia taratibu
na miongozo ya matumizi ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi hiyo, huku
akibainisha kuwa haikubaliki.
Aliwaagiza na kuwataka wasimamizi wa
miradi ya matengenezo ya barabara kuzingatia taaluma na weledi husika ili
kupata thamani ya fedha kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu husika bila
kukiuka sheria ya manunuzi.
Temeke
Aidha, wakati wakijadili nafaniki na
mipango ya maendeleo kwa upande wa Temeke, Sadiki alimuagiza Mkurugenzi wa
manispaa hiyo hadi ifikapo Jumatatu ijayo ahikikishe anamfikishia taarifa
kuhusu maeneo yote ya wazi ambao umiliki wake hauweleki.
Alisema maeneo hayo yanadaiwa kuwa yana
wamiliki wake lakini cha kushangaza kwa muda mrefu hayajaendelezwa huku
serikali Manispaa ikikosa maeneo kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wananchi.
“Niwapongeze Temeke kwa hatua yenu ya
kununua mashine kubwa kwa ajili ya kufanyia usafi hata hivyo jaribuni kusimamia
miradi mingine ili iweze kukamilika,”alisema Sadik.
Mkuu wa wilaya hiyo Sofia Mjema,
aliiomba Wakala wa Barabara Tanzania
(Tanrods) kukamilisha barabara zote ambazo wamezianza kwani iko baadhi ya
miradi imechukua muda mrefu bila ya kukamilika kwa wakati.
Kinondoni
Kwa upande wa wilaya hiyo, Sadiki alimuagiza
Mkurugenzi kuwa anahakikisha kuwa anasimamia shuguli ya kuwadhibiti watu wote
wanaotaka kurejea katika maeneo ya mabondeni baada ya kuondolewa hivi karibuni.
“Maeneo
haya ni hatarishi hivyo ni lazima mhakikishe kuwa kila aliyeondolewa katika
maeneo hayo harejei tena, na ieleweke serikali haina uwezo wa kuwapatia viwanja
wananchi hao kwani ni gharama kubwa,”alisema Sadiki.
Sadik,
alitoa msimamo huo baada ya Wabunge Bonah Kalua na Maulid Mtulia kuitaka
serikali kuwasaidia viwanja wakazi hao kwa vile ni masikini na wanahitaji
msaada.
Pia,
aliagiza uongozi wa Halimashauri hiyo kuwa inawaondoa wafanyabiashara
ndogondogo katika eneo la ubungo na kuwapeleka katika Kituo cha Mabasi Simu
2000.
“Nashangaa
kituo kile kimetumia mamilioni ya shilingi lakini nashangaa mnakataa kukitumia,
hakikisheni mnawaondoa kwani ni hatari kwa wafanyabiashara hao wanaoning’iniza
biashara zao kweye mashine ya kupoozea umeme (transphomer),”alisema Sadiki.
Ilala
Mkuu huyo wa Mkoa, baada kusikiliza matatizo
ya uharibifu wa barabara za Halmashauri, unaofanywa na baadhi ya magari yenye
uzito mkubwa wa ukilinganisha uwezo wa barabara hizo zenye uwezo wa kuhimili
uzito wa tani saba, kwanza aliomba alezwe ni nani anahusika katika utoaji wa
vibali kwa gari hizo kuungia katikati ya jiji.
Hata
hivyo, Wakurugenzi pamoja na watendaji wao wote walishindwa kumtaja mhusika,
hali iliyomfanya atowe uamuzi mgumu ambao ulikuwa ni kufuta vibali vyote vyote
vinavyoruhusu gari zenye uzito wa zaidi ya tani kumi.
Alisema
kuanzia jana mtu yeyote, atakayekaidi agizo hilo atakuwa amevunja sheria hivyo hatua kali
za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Aliwataka
wakurugenzi na watendaji wake wote kuwa wakali katika kusimamia hilo kwani bila ya
kufanya hivyo barabara za halimashauri zitaendelea kuharibika hukku wakiendelea
kuiomba serikali msaada.
“Halmashauri
zote hakikisheni magazri hayo yenye uzito zaidi ya tani kumi hayapiti kwenye
barabara zetu za halmashauri hii itatusaidia kuzuia uharibifu,”alisema Sadiki.
Awali Mbunge
wa Ilala, Mussa Azan Zungu, alisema uharibifu huo ulikuwa ukichangiwa na
utolewaji vibali vya magari yenye uzito mkubwa kuingia katika barabara uwezo wa
kuhimili uzito wa kuanzia tani tano hadi kumi.
Alisema, kama hakutakuwa na ushirikiano wa kusimamia miundombinu
hiyo ya halmashauri za wilaya basi zitaendelea kulalamika huku barabara hizo
zikiendelea kuharibiwa.
No comments:
Post a Comment