KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Wednesday, 30 March 2016

OFISA USAFIRI MUHEZA MATATANI

OFISA Usafirishaji wa Manispaa ya Halmashauri ya Muheza, George Masatu, ameingia matatani baada ya kudaiwa kutumia magari mawili ya ofisi kwa ajili shughuli zake binafsi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya halmashauri hiyo kilidai kuwa serikali inapaswa kudhibiti matumizi ya magari hayo kwa kuwa kimekuwa chanzo cha kuongezeka kwa matumizi ya serikali.
Kilidai kuwa matumizi ya ofisa huyo yamechangia gharama za uendeshaji wa magari hayo hususani matumizi ya mafuta.
Chanzo hicho kilitaja magari yanayotumiwa katika shughuli za ujenzi wa nyumba ya ofisa huyo ni SM 5581 na SM 3924 Toyota pickup.
“Kama serikali inapambana ili kudhibiti mishahara hewa katika halmashauri zetu basi pia itambue kuna jipu jingine linaloongeza matumizi ni shughuli binafsi za baadhi ya maofisa kama Masatu,” kilidai.
Akizungumzia tuhuma hizo Masatu alisema ndiyo kwanza anazisikia taarifa hizo hivyo hawezi kuzungumzia chochote huku akidai kuwa taarifa hizo zinatokana na chuki binafsi.
“Wakati mwingine hebu tujiongeze, hivi kweli gari hizo zinaweza kubeba mzigo mzito, acha nikwambie kuwa sijawahi na sitajafanya kitendo hicho,” alisema Masatu.

Masatu aliwashangaa waliotoa taarifa hizo na kuwaita kuwa ni watu wenye chuki binafsi kwani uhusiano wake wa kikazi na wafanyakazi wenzake ni mzuri.

No comments:

Post a Comment