KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Thursday, 3 March 2016

TPA YAFAFANUA UNUNUZI WA MATISHARI MATATU TANGA



MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema ununuzi wa wa matishari tatu kwa ajili ya upakiaji na upakuaji mizigo katika Bandari ya mkoani Tanga, ulipata baraka zote za Bodi ya Wakurugenzi.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, na kusainiwa na Menejmenti ya TPA, ilieleza kuwa mchakato wa kununua matishari hizo ulianza mwaka 2010/11 baada ya aliyekuwa Mkuu wa Bandari kwa wakati huo, kuandika barua kwa Mkurugenzi Mkuu kukunuliwa matishari hayo matatu ya tani 300.
Kwa mujibu wa Menejimenti matishari hayo, yalinunuliwa baada ya shehena ya mizigo kuongezeka katika bandari hiyo ya Tanga.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa matishari hayo yalinunuliwa baada ya maombi ya kuzinunua kupitishwa na Bodi ya Wakurugenzi, wa viwango vya ubora (Technical Specification).
“Uamuzi ulipitishwa kwa ajili ya ununuzi wa tishari (barges) mbili, viwango viliandaliwa na Kurugenzi ya Uhandisi na kuwasilishwa katika Kitengo cha Ununuzi kwa ajili ya kuanza mchakato wa zabuni Februari 2011,”ilieleza taarifa hiyo.
Aidha, tangazo la zabuni ya ununuzi wa matishari lilitoka Februari 28, 2011 na Machi Mosi kupitia magazeti ya the Guardian na Machi Mosi, 2011, likatoka kwenye gazeti la serikali Daily News, Machi Mosi na Mbili mwaka huo huo wa 2011.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa ilipofika Aprili 28, 2011 zabuni zilifunguliwa na jumla ya wazabuni nane walijitokeza kwa kupeleka maombi yao.
Baada ya ufunguzi wa zabuni Kamati ya Uchunguzi  wa Zabuni iliundwa na Mkurugenzai Mkuu na ilijumuisha ‘Marine Engineer’ kutoka Bandari ya Tanga ambaye kwa kipindi hicho alikuwa amehamishiwa Bandari ya Dar es Salaam.
Ilifafanua kuwa baada ya uchambuzi wa zabuni kukamilika Bidi ya Zabuni, iliamriwa kwamba Kamati ya uchunguzi iundwe ili kwenda kufanya ‘due diligence’ kwenye kiwanda cha mzabuni aliyependekezwa kufanya kazi hiyo kabla ya kupewa zabuni hiyo.
Baada ya uchunguzi Kamati hiyo ya uchunguzi ilifanyakazi yake na kupeleka taarifa kwamba walijiridhisha kuwa kampuni hiyo ilikuwa na uwezo wa kufanya kazi hiyo.
Menejimenti hiyo, ilifafanua kuwa baada ya uchambuzi huo wa kina pamoja na kupitia taarifa ya uchunguzi, Bodi hiyo ya Mamlaka ya Bandari iliidhinisha zabuni kutolewa kwa kampuni itwayo John Achelis anda Sohne Gmbh ya Ujerumani katika kikao chake maalum Na. 135 kilichafanyika Desemba Mosi na Mbili mwaka 2011.
Ilieleza kuwa Januari 10 mwaka 2012 Mkurugenzi Mkuu alitoa barua ya kupewa John Achelis anda Sohne Gmbh, kwa ajili ya kutengeneza matishari matatu ya ukubwa wa tani 3500 kila moja kwa gharama ya dola za Kimarekani 10,113,00.
Makubaliano hayo yalikuwa matishari hayo yatengenezwe kwa na hatimaye mkataba wa manunuzi wa matishari hayo ukasainiwa ukasainiwa mnamo Machi 2, 2012. 
Baada kikao hicho mkataba ulisainiwa, Mshitiri (Supplier), alipeleka michoro kwa ajili ya kutumika katika ujenzi wa matishari hizo huku akiomba uidhinishwe na mamlaka ya bandari kabla ya kuanza utengenezaji.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa michoro hiyo iliidhinishwa na Mkurugenzi wa Uhandisi. 
Kulingana na mkataba matishari hayo yalitakiwa yajengwe kwa kuzingatia ubora wa kimataifa chini ya usimamizi wa Bureau ‘Veritas’ (B/V) na yalijengwa kwa ubora huo na kuidhinishwa na B/V.
Aidha, Mshitiri alitakiwa kusafirisha matishari hayo kwa kupakiwa katika meli, hata hivyo matishari hayo hayakupakiwa kwenye meli na baadala yakeyalivutwa kwa kutumia boti kwani John Achelis and Sohne Gmbh.
Mshitiri aliomba kubadili kubadilisha njia ya usafirishaji kuwa wa kuvutwa kwa boti baadala ya kupakiwa kwenye meli na TPA iliridhia matishari hayo yavutwe baadala ya kupakiwa melini na yalikatiwa bima ya kusafirisha kwa njia hiyo.
Wakati wa usafirishaji njiani yalikumbana na dhoruba ya kimbunga kikali baharini na kusababisha boti iliyokuwa ikiyavuta matishari hayo kuzama na kufanya matishari hayo kugongana kwa kupigwa na mawimbi na kusukumwa hadi nchini Malaysia yalipokwama kwenye tope na mikoko.
Ilieleza kuwa ajali hiyo ilisababisha matishari hayo kupata uharibifu.
Kwa kuwa maishari hayo yalikatiwa bima, ya kusafirisha kwa njia ya kuvuta na yakapata ajali iliyosabaisha uharibifu huo, gharama za matengenezo ya matishari hayo zikabebwa na bima iliyokatwa.
Kabla ya matengenezo hayo kufanyika Surveyor wa B/V, alifanya ukaguzi wa uharibifu na kuruhusu matengenezo yafanyike kwa kila tishari kulingana na uharibifu wake.
Taarifa hiyo inaonesha wakati wa matengenezo wataalamu wa TPA walifanya ukaguzi mara mbili wakati matengenezo hayo yakiendelea na pia baada ya utengenezaji kukamilika na kuridhiwa na Mkaguzi B/V.
Baada ya matengenezo hayo, matishari hayo yalivutwa na kuletwa bandari ya Tanga Agost mwaka 2014 na baada ya kufanyiwa ukaguzi yalionekana kuwa na kasoro chache kama vile kutokuwepo na fenders zenye uwezo wa kuzikinga wakati wa maegesho melini ama gati.
Pia yalikuwa hayana mifuniko ya Falk ‘Hatch’ kuwa si rafiki katika shughuli za kupakia na kupakuwa, na Mshitiri alitakiwa kufanya marekebisho kwa gharama zake kwa kuwa tishari hizi zilikuwa bado hazijajaribiwa na kupokelewa na TPA.
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa baada ya kufanyiwa majaribio yalfanywa, Agosti 3, 2015 kwa kupakia shehena ya coal toka kwenye meli ya African Griffon.
Katika mkataba ilielewekwa wazi kuwa matishari hayo yakifika Tanga yafanyiwe majaribio ili kuangalia uwezo na tabia ya matishari hayo yakiwa ya yamejazwa shehena.
Majaribio hayo yalionesha kuwa matishari hayo yalikuwa imara wakati yalipopakiwa mizigo na kuweza kuvutwa hadi kwenye gati na kupakuliwa mzigo huo.
Taarifa hiyo, ilieleza kuwa matishari hayo yaliendelea kufanyiwa majaribio kwa kuhudumia meli tatu ambazo ni African Griffon iliyofika bandarini Tanga Agosti 31, 2015, Diamomond Sky  Desemba 04, 2015 na Thor Breeze iliyofika Januari 12, 2016.
“Wakati matishari hizo yakifanya majaribio matatizo yafuatayo yalijitokeza wakati wa upakuaji wa shehena, ambazyo ni ukubwa wa matishari umesababisha krini za meli kushindwa kupanga mizigo vizuri hivyo kulazimu kuhitajika kwa ‘wheel loaders’ ambazo tayarimchakato wa ununuzi wake umeanza.
Tatizo jingine ni Tug Boat’ kubwa inahitajika kwa ajili ya kukokota matishari hayo na tayari mamlaka imeagiza na inatarajiwa kuwasili Tanga Juni mwaka huu.
Kutokana na matatizo yaliyojitokeza Mshitiri alitakiwa kurekebisha ‘hatch cover’ kama ilivyokubalika wakati wa majaribio na ndiyo maana hadi sasa hajalipwa kiasi chake cha fedha ambacho ni dola za Marekani 1,348,400.
Kwa mujibu wa mkataba kiasi kilichobaki kinapaswa kulipwa baada ya majaribio kufanyika kwa mafanikio na kupewa ‘Certificate Acceptance’ ambayo hadi sasa hajapatiwa.
Taarifa hiyo inaonesha kuwa TPA inapenda kuwahakikishia watumiaji wa Bandari kwamba inaendelea kuboresha miundombinu na vifaa ili kutoa huduma zilizo bora na za viwango.

No comments:

Post a Comment