BAADHI ya
wazazi wenye watoto wanaosoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya
Binti Mussa, wilayani Ilala, wako mbioni kuwahamishia watoto wao katika shule nyingine,
kwa madai ya wanafunzi hao kutofundishwa masomo ya Siyansi tangu walipojiunga
na muhula wa masomo mwaka huu.
Halikadhalika wazazi
hao wameushutumu uongozi wa shule hiyo kwa kushindwa kusimamia vizuri michango ya wazazi kwa ajili ya kununua madawati hadi
kusababisha wanafunzi kukali visafleti vilivyojazwa mchanga kama madawati.
Naye Mkuu wa
Shule hiyo Fadhil Mbata amesema wazazi wanaodai hivyo ni wale wasiyopenda
kuhudhuria vikao vya wazazi vyenye lengo la kujadili maendeleo ya shule hiyo.
Hayo yalisemwa
na wazazi jijini Dar es Salaam leo, wakati walipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kuhusu malalamiko
hayo ambayo hivi sasa yamefikia hatua mbaya ambayo inaweza kuangusha kiwango
cha ufaulu wa watoto wao.
Mmoja wa zazi
hao, Khamis Juma, alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa chanzo cha
matatizo hayo kinachangiwa na Mkuu wa
Shule hiyo ambaye ameshindwa kuwalipa walimu wanaofundisha masomo hayo kwa
mkataba.
Alisema,
kutokana na mazingira hayo wameona ni vema wakawamisha watoto wao kwenda katika
shule wanazoamini kuwa watoto hao watafundishwa na kujihakikishia ufalu wao
katika mitihani yao.
Juma alisema
hivi sasa watoto hao wanakabiliwa na mtihani kwa ajili ya mapuniziko mafupi ya
mwezi watatu lakini cha kushangaza wanafunzi hao tangu walipojiunga na muhula
wa masomo ya kidato cha kwanza mwaka watoto hao hawajafundishwa somo la bioloji
kiasi hawajui siku ya mtihani watajibu nini.
Aidha, baada ya
Mkuu huyo wa Shule hiyo kuona wimbi la wazazi kuhamisha watoto linaongezeka hivi
sasa ameamua kuzuia utaratibu huo kwa kuwaeleza wazazi kuwa Ofisa Elimu wa
Wilaya amepiga marufuku uhamishaji huo wawatoto katika shule hiyo.
“Kwa mfano kuna
mwalimu aliyekuwa akifundisha somo la Bioloji na ambaye ameisaidia ufaulu wa
somo hilo katika mtihani uliyopita lakini cha ajabu mwalimu huyo hajalipwa malipo
yake kwa zaidi ya mwaka haliyomfanya ashindwe kuendelea na kufundisha somo
hilo,”alisema Juma.
Alisema baada
ya Mkuu huyo kuona deni la mwalimu huyo linazidi kukuwa ikabidi aachane na
mwalimu aliyekuwa akifundisha somo hilo la bioloji huku akiamua kufundisha masomo
yote ya sayansi huku akikabiliwa na majukumu ya uongozi kitendo kinachomfanya
ashindwe kuingia darasani kwa wakati.
Hata hivyo,
pamoja nakuogopa deni la mwalimu huyo kukuwa, sasa ameamua kufanya ujanja wakufundisha
masomo hayo, huku akiandika madai ya kulipwa kama vile mwalimu wa mkataba
jambolo linamfanya awakoseshe vipindi wanafunzi hao.
Madawati
Naye Fatuma
Charles, alisema kuwa uongozi wa shule hiyo unaongoza kwa matumizi mabaya ya
michango ya madawati kutoka kwa wazazi ambao walijitolea kuchangia katika
kipindi cha mwaka 2013 hadi mwaka jana.
Alisema baada
ya kushindwa kutumia michango hiyo vizu, kumefanya watoto kukalia viroba walivyovijaza
mchanga kama vile ndiyo madawati.
“Kuna wenzetu
wanahamisha watoto wao lakini mimi nasema sitamhamisha mwanangu bali
nitapambana na uongozi wa shule kwa lengo la kuisaidia shule hii kwa sababu
kumhamisha mtoto siyo ufumbuzi wa tatizo na vipi kwa wale wasiyokuwa na uwezo
watafanyaje,”alisema Fatuma.
Akizungumzia
malalamiko hayo, Mkuu wa Shule hiyo, Mbata
alisema kuwa kukosekana kwa walimu hao wa sayansi kumetokana na wazazi wenyewe
kushindwa kulipa madeni ya walimu hao waliyokuwa wakifundisha masomo hayo ya
zaiada (Parttime).
Alisema kuingia
kwake kwenye vipindi siyo kama amejirundikia vipindi ama anajilipa bali anaingia
kwa dharula na hiyo intokana yeye kupenda kuona watoto hao wanakaa darasani
bila ya kufundishwa.
Mbata, alisema
kutokana na mazingira hayo hata weza kuendelea na kuingia darasani ila alichofanya
ni kupeleka taarifa kwenye ngazi husika
kwa ajili ya kuongezewa walimu ambapo hatua za utekelezaji zimekwishaanza.
“Suala la ngono
kati ya wanafunzi na walimu kama mzazi ana taarifa za kutosha basi azifikishe
kwenye kamati ya shule ili mhusika achukuliwe hatua hivi kama mwalimu anafanya
hivyo basi huyo hana sifa tena ya kuitwa mwalimu ni wakufukuzwa tu,”alisema
Mbata.
Akizungumzia
madawati, Mbata, alisema michango ya wazazi imetumika kama ilivyokusudiwa na
wala siyo kweli kama kuna wanafunzi wanakalia viroba vilivyojazwa mchanga
ingawa kweli hapo awali yalikuwepo matatizo hayo.
No comments:
Post a Comment