KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Monday, 18 April 2016

MAGUFULI AVAMIA CRDB (HOLLAND BRANCH)



RAIS John Magufuli amezua mjadala baada ya kuvamia Tawi la CRDB (Holland Branch), akiwa kwenye gari namba T 182 DFQ huku likiwa halina nembo ya adamu na hawa wala bendera.
Tukio hilo lililochukuwa dakika 25, limetokea majira ya asubuhihi jijijni Dar es Salaam jana katika tawi hilo ambalo liko katika makutano ya Barabara ya Ohio na Samora bila kutarajiwa.
 Mara baada ya Rais Magufuli kufika katika eneo liliko tawi hilo makutano ya barabara hizo yalifungwa huku ndipo rais aliposhuka kwenye gari  na kuingia ndani ya benki hiyo.
Wakati akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliyokuwa awakijiandaa kuingia ndani ya benki hiyo ilibidi wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao waliyokwisha ingia.
Aidha, baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais kuingia benki kwa sitaili ile kwani baadhi ya wananchi kudai kuwa hawajaona tukio kama lile kwa marais wote waliyopita.
James Charles, ambaye ni dereva wa Tex, alisema baadhi ya wananchi waliyokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimalishwa walishtuka lakini mara walimuona Rais Magufuli akishuka kwenye gari hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea ofisi yake ya zamani.
“Lakini kufumba na kufumbua tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB tukajiuliza vipi rais leo kaamua kuwa kama mteja hata hivyo hatujui kama hiyo ilikuwa inawezekana.
Lazima kutakuwa na kitu haiwezekani aende akachukue fedha kwa utaratibu ule ngoja tusubiri tutasikia amefuata nini,”alisema Charles.
Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi wa moja ya chuo kimoja cha elimu ya juu, alisema kuja kwake kumewashtua wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani anadhani wanadhani rais alikwenda pale kwa ajili ya kutumbua majipu.
“Mimi nwakati Rais Magufuli anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri huduma kwa ujumla kila mmoja wetu alishituka lakini hatukujua kilichomleta,”alisema.
Wandishi,wali jaribu kutaka kujua kilichompeleka Rais Magufuli pale kwa kuwauliza baadhi ya wafanyakazi wa tawi hulo hata hivyo hakuna aliyekuwa tayari kuzungumzia ujio huo kwani nao hawakuwa wakijua chochote.
Baada ya Rais Magufuli kumaliza kazi yake iliyompeleka alitoka na kuingia kwenye gari lake kisha wakati akiondoka alishusha kioo huku akichungulia nje na kuwapungia mkono wananchi.

No comments:

Post a Comment