KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Tuesday, 19 April 2016

TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO CHAPOKEA MSAADA WA SH.MILIONI 80




KITUO cha Utamaduni na Maendeleo cha Denmark (CKU), kimetoa msaada wa vifaa vya muziki katika Tasisi ya Sanaa na utamaduni Bagamoyo (TASUBA), vyenye thamani ya sh. milioni 80 za kitanzania.
Mbali na kununua vifaa vya muziki, sehemu ya fedha hizo piazitatumika katika matengenezo 
na uangalizi wa vifaa hivyo katika kipindi cha mwaka mmoja wa mradi huo.
Akizungumza jana wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Msimamizi wa Program wa CKU hapa nchini, Mandolin Kahindi, alisema msaada huo kuwa ni moja fursa ya kuendeleza utamaduni kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi.
Alisema, kuwa msaada huo ni utekelezaji wa mpango wa utamaduni na ubunifu wa Tanzania unaotekelezwa na kituo hicho kwa ushirikiano na ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.
"Unajua  mpango wa kuanza kutoa msaada kwa Tasuba ulianza mwaka 2014 baada ya CKU kukitembelea chuo hicho na kuelezwa kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa vifaa vya muziki kwa ajili ya  mafunzo na kujifunzia"alisema.
Alifafanua kuwa mpango huo wa kusaidia uliazinduliwa rasmi Juni mwaka jana, ulilenga kutengeneza fursa za kiuchumi kupitia jukwaa la sanaa na ubunifu ambapo watanzania watajipambanua kupitia kushiriki shughuli mbalimbali za kitamaduni na kujipatia kipato.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Leah Kihimbi, alisema kuwa amefurahi kupata msaada huo katika chuo cha sanaa lengo likiwa ni kuendeleza vipaji hapa nchini.
"Unaju katika chuo hii ni kweli kulikuwa na uhaba wa vifaa vya kufundishia lakini sasa tumepokea msaada kutoka katika Danish Centre for Culture and Development(CKU), kuweza kuwaidia wanafunzi katika chuo hiki.
Aliongeza na kusema kuwa ni jambo la kuigwa kwa tasisi nyingine lengo ni kuweza kusaidia vyuo mbalimbali hapa nchini. 

No comments:

Post a Comment