BAADHI ya wakazi wa Jiji la
Dar es Salaam wameomba serikali kutoa ufafanuzi kuhusu ubomoaji wa vipande vya
Barabara ya Mradi wa Magari ya endayo Haraka (DART) vilivyokamilika, kitendo
kinachosabaisha foleni za mara kwa mara.
Hayo yalisemwa jijini Dar
es Salaam leo, wakazi hao wakati walipokuwa wakizungumza na BLOG hii katika
eneo la Kimara Mwisho.
Kwa niaba ya wenzake,
Charles Simon, alisema hawelewi kuna tatizo gani ambalo linafanya mafundi hao
wawe wanabomoa vipande vya barabara hiyo vilivyokamilika.
“Unajua Watanzania sisi ni
watu wa ajabu sana kila kinachofanyika kiwe ni kizuri au kibaya hakuna anayehoji,
angalia barabara hii kuna maeneo yamekamilika kabisa lakini ghafla tunaona yanabomolewa
na kusabisha usumbufu kwa watumiaji wake lakini tuko kimya,”alisema Simon.
Alisema, wanahitaji
waelezwe kinachosababisha barabara hiyo kubomolewa mara kwa mara kunasababishwa
na nini, pia wajue kama ni uzembe serikali inamchukulia hatua gani mkandarasi.
Aidha, alisema mkandarasi
huyo kama ataachwa aendelee na utaratibu huo wa kujenga na kubomoa
kunauwezekano ujenzi huo ukashindikana kukamilika kwa wakati hali itakayowafanya
watumiaji wa barabara hiyo kuendelee kuteseka na msongamano unaojitokeza mara
kwa mara.
Aliyataja baadhi ya maeneo
yaliyokumbwa na ubomoaji huo kuwa ni yale ya Kimara Fire na Akiba (kwenye
makutano ya barabar ya Morogoro na Bititi).
Katika hatua nyingine
wakazi hao pia wameiomba serikali kutekeleza kwa vitendo katika kuwakamata
baadhi ya madereva wa magari na bodaboda ambao wamekuwa wakijihusha na vitendo
vya wazi vya kuharibu barabara hiyo.
Simon, alisema ni jambo la
kushangaza kwa madereva hao kushindwa kuwa na uvumilivu pindi inapotokea
foleni, wao huamua kupanda kwenye maeneo amabyo kisheria hayaruhusiwi kupita
matokeo yake ni kuharibu barabara hiyo.
“Tumesikia mara kadhaa kuwa
kila anayejihusisha na uharibifu huo atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya
sheria lakini cha kushangaza uharibifu huo unaendlea lakini hadi leo hakuna
hata dereva mmoja aliyekwisha kamatwa na kufikishwa kwenye vyombo hivyo vya
sheria.
No comments:
Post a Comment