MKURUGENZI wa Takwimu za Uchumi, Morice
Oyuke, amesema pato la Tifa katika robo kipndi cha robo ya tatu ya mwaka 2014
limeongezeka kwa kasi ya asilimia 6.8 ikilinanishwa na asilimia 7.4 mwaka 2013.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Oyuke, alisema
takwimu hizo zilizowasilishwa jana ni za Julai hadi Septemba, kwa bei za miaka
inayohusika na mwaka wa 2007, ambazo zinasambazwa kwa mara ya kwanza.
“Hizi ni kwa kuzingatia marekebisho ya
takwimupato za pato la taifa kwa bei za mwaka 2007,”alisema Oyuke.
Alisema, kupanda kwa takwimu hizo za
pato la taifa kulitokana na ongezeko la ukuaji wa nishati ya umeme kulikotokana
na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme unaotokana na mafuta na gesi.
Oyuke, alisema, takwimu hizo za pato la
taifa hupimwa kwa kuangalia thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa nchini
katika vipindi vya miezi mitatu, mitatu ambavyo ni Januari hadi Machi, Aprili
hadi Juni, Julai hadi Septemba na Oktoba
hadi Desemba.
“Utayarishaji wa takwimu za pato la
taifa hujumuisha shughuli zote za kiuchumi na hivyo hutumika katika
kutathimini, mipango na kutayarisha sera za kiuchumi,”alisema Oyuke.
Aidha, shughuli nyingine kama vile
huduma za malazi na chakula zilikua kwa kasi ya 0.2 ikilinganishwa na asilimia
hasi 0.4, shughuli za habari na mawasiliano nazo zilikuwa kwa asilimia 11.9
katika robo mwaka ya tatu 2014 ikilinganishwa na asilimia 7.0 mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment