KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday, 15 March 2015

CHADEMA UKONGA YASAIDIA MSIKITI

KATIBU wa zamani wa Jimbo la Ukonga (Chadema), Juma Mwipopo amewataka viongozi  Wa dini  kuwahamasisha waumini wao kwenda kujiandikisha  kwenye daftari la wapiga kura kawani bila ya kufanya hivyo haki yao ya kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu itapotea.


Sambamba na hilo pia wahakikishe kuwa kipindi cha kupiga kura kikifika wahakikishe kuwa waumini hao wanapiga kura  bila kukosa.

Wito huo aliutoa juzi jijini Dar es Salaam juzi, wakati Katibu Baraza la wanawake Jimbo hilo, Asia Msangi (Chadema), alipokuwa akikabidhi msaada wa mifuko 13 ya saruji kwa viongozi  wa misikiti ya Salama  na Takwa iliopo mtaa wa Kipunguni ‘B’ Kata ya Kivule.

"Hawa ni viongozi ambao wanakundi kubwa la watu ambao wanaowahaeshimu baadala ya kuichia serikali jukumu pekee yake,"alisema Mwipopo,

Mwipopo alisema  kuna haja ya viongozi wa dini nao wakajitokeza na kuchangamkia kugombea nafasi mbalimbali hususani udiwani, Ubunge na hata urais,  kwa kuwa asilimia kubwa ya wananchi wanawaamini sana viongozi hao.

“Tunawaomba pia viongozi wa dini wagombee nafasi mbalimbali  wananchi watawaamini na watawachagua kwa kuwa viongozi hawa wanaaminiwa na wananchi ”alisema.

Katibu  wa Baraza   la wanawake Jimbo hilo, Asia Msangi akikabidhi msaada huo, alisema wakati umefika  sasa wa kusaidia nyumba za ibada kutokana na nyumba hizo kukabiliwa na changamoto mbalimbali.

“Ninamkakati wa kuendelea kuboresha nyumba za ibada, kutoa misaada kwa watoto yatima, nasikitishwa na watu  wanaoweka vipau mbele  katika kuchangia sherehe  na kusahau vitu vya muhimu kama nyumba za ibada”alisema Msangi.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi waliopokea msaada huo, Shaban Omary  ambaye ni imamu wa Msikiti wa  Masjidi Takwa , alisema msaada huo usiwe mwisho bali uwe ni chanzo pia  uwe ni kichocheo kwa watu wengine.

No comments:

Post a Comment