BENK ya Stanbic Tanzania
imezindua huduma za kibenki kwa njia ya mtandao wa kieletronikali HIVI KARIBUNI
zinazowawezesha wateja kupata huduma kupitia simu za mkononi au kwenye kompyuta
zao binafsi.
Uzinduzi wa huduma hii mpya ni
mkakati wa kuwapatia huduma wateja kwa urahisi hususani wanaotumia simu za
mkononi ikizingatiwa kuwa utumiaji wa
simu hizo umekuwa kwa kiwango cha asilimia 80 barani Afrika na unazidi kukua
hali inayotia matumaini kuwa siku za usoni huduma za kibenki zitawafikia
kirahisi wananchi wengi wanaoishi maeneo ya vijijini ambao wengi wao kwa sasa
hawanufaiki na huduma za kibenki.
Kwa sasa mabenki na taasisi
mbalimbali za kifedha zimeanza mkakati wa kusambaza huduma zake ili ziwafikie
wananchi wengi zaidi hususani wanaoishi maeneo ya vijijini kupitia huduma za
mtandao wa kielectronikali, pia huduma
hizi zinawarahisishia wananchi wanaoishi mijini kupata huduma za kibenki na
kuepukana na kupoteza muda wao mwingi kupanga foleni kwenye mabenki
wanapohitaji kupata huduma.
Benki ya kimataifa ya Stanbic
ambayo asili yake ni barani Afrika kwa hapa Tanzania imeanza kutoa huduma hii
mpya kwa wateja binafsi na wateja wa makampuni na itawarahisishia maisha wateja
wake ambao wataweza kupata huduma za
kibenki na kufanya mihamala ya malipo wakiwa majumbani kwao ka katika sehemu
zao wanazofanyia biashara.
Akizungumzia huduma hiyo mpya
Farha Mohammed,Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Benki kwa njia ya mtandao wa
Stanbic Tanzania
amesema :
“Tumeanzisha huduma hii kuwarahisishia maisha wateja wetu ambao kwa sasa wanaweza
kupata huduma kwa urahisi na huduma hii ni salama,inaaminika na ni rahisi
kuitumia hata kama mtumiaji anaitumia kwa mara ya kwanza,tumedhamiria kuondoa
usumbufu wa kupata huduma za kibenki kwa wateja wetu”
Alisema wanachotakiwa kufanya wateja ni kujisajili kwa njia
ya mtandao kwa kutumia vitambulisho vyao vyenye maelezo yanayowahusu.
Baada ya kujisajili mteja anaweza kuangalio salio kwenye
akaunti yake,viwango vya ubadilishanaji fedha za kigeni vya siku,taarifa za
akaunti yake,kununua umeme wa LUKU ,kulipia ankra ya maji na kununua muda wa
maongezi wa simu na kadhalika.
No comments:
Post a Comment