![]() |
| Waziri wa Ujenzi, John Magufuli |
BAADHI ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wameitaka
Wizara ya Ujenzi kutoa ufafanuzi kuhusu stendi za mradi wa Mabasi yaendayo
Haraka (DART), kujengwa kwa kutumia mbao na nyavu kama vile mabanda ya kuku.
Wakazi hao, walisema hivyo kutokana na maelezo kuwa
stendi za mradi huo zingejengwa kisasa zaidi kwa kutumia vioo na teknolojia
inayokwenda na mfumo wa kidigital.
Walisema pamoja na matumizi hayo ya mbao, kibaya zaidi
mbao hizo zinaonekana kuwa dhaifu na kwamba zinaweza kuharibika kwa muda mfupi.
“Tunaomba ufafanuzi mapema ili likija kutokea la kutokea
wahusika wasije kukwepa ubadhilifu wanaoufanya, tumebaini katika hatua hizi za
mwisho kuna maeneo yanajengwa chini ya kiwango mfano ni uwekwaji wa hizi mbao
na nyavu ambazo hazifanani kabisa na mradi wenyewe.
Walizitaja baadhi ya stendi hizo kuwa ni zile za kuanzia
Kimara mwisho ambazo ni Bucha, Baruti, Kona na nyigine.
Wakazi hao walisema wanawasiwasi kuwa huenda mipango
iliyokusudiwa awali ikawa imeishaanzwa kuvurugwa na baadhi ya watu wenye taamaa
ya fedha.
Waliendelea kusema kuwa ni vema Waziri wa Ujenzi John
Magufuli akafanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo, kisha atoe
ufafanuzi kama ujenzi huo ulipangwa kuwa wa aina hiyo, itasaidia kuwatoa
wasiwasi wananchi.

No comments:
Post a Comment