KAMA UNA TUKIO LOLOTE LA KIJAMII, SIASA, UCHUMI TUWASILIANE KWA E-mail: shehesemtawa@gmail.com SIMU: 0719 352 268

Sunday, 15 March 2015

OBRIGADO KUTUA TAMASHA LA PASAKA 2015

Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kuhusiana na ujio wa mwimbaji nyota kutoka Afrika Kusini Thori Mahlangu (Obrigado). (Picha Francis Dande)
Na Loveness Mboje
RAIA  wa Afrika Kusini
ambaye ni Mwanamziki wa nyimbo za injili, Thori Mahlangu (Obrigado),
amethibitisha kuwa mmoja wa waimbaji wa kimataifa watakaotumbuiza katika
Tamasha Pasaka litakalofanyika Aprili 5.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha
hilo, Alex Msama alisema kuwa sambamba na mwimbaji huyo ataambatana na waimbaji
wengine 16 kutoka nchini humo huku Faustine Munishi maarufu kwa jina la Malebo na
Solomon Mukubwa  kutoka nchini Kenya nao watakuwepo.
Msama alisema kuwa viingilio vya tamasha hilo kwa watoto vitakuwa shs. 2,000 viti vya kawaida shs.5,000 VIP B, shs. 10000 VIP A shs. 20,000 kwa watu wakubwa na kuongeza kuwa mara baada
ya tamasha hilo, Aprili 12 itakuwa ni zamu ya wakazi wa jiji la Mwanza katika Uwanja wa  CCM Kirumba.
Aidha kwa upande wa waimbaji wazawa  Msama amesema kuwa mwimbaji Joshua Mlelwa ambaye alikuwa
mwimbaji wa Upendo Group  naye atapamba tamasha hilo ambalo linasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki.
Tamasha hilo linatimiza
miaka 15 tangu lianzishe na linatarajiwa kihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka
nchi za Kenya, Uganda,Rwanda, Afrika Kusini Uingereza na
wenyeji Tanzania.

No comments:

Post a Comment